1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Kinga dhidi ya ugaidi iimarishwe

23 Machi 2016

Magaidi wanataka kuona tukisalimu amri. Kamwe hilo halitatokea. Na baada ya kuomboleza vifo vya raia wasio na hatia, mapambano dhidi ya itikadi kali laazima yaimarishwe, anasema mwanadishi wa DW Brussels, Bernd Riegert.

https://p.dw.com/p/1IHzB
Belgien Je suis Bruxelles Schriftzug
Picha: DW/B. Riegert

Huo ulikuwa mshtuko mkubwa. Magaidi wameulenga moyo wa Ulaya - na wameacha athari. Watu wasio na hatia wameuawa, mamia wamejeruhiwa. Ni vurugu zisizokuwa na mantiki. Ni uso wa kuogofya wa ugaidi wa itikadi kali za Kiislamu mjini Brussels. Ubelgji ilikuwa kwanza ndiyo inapata ahueni baada ya kufanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba mjini Paris siku ya Ijumaa. Na sasa.

Lango la Brandeburg la mjini Berlin na mnara wa Eifel mjini Paris vitapambwa na rangi za benera ya taifa ya Ubelgji. Wakaazi wote wa Ulaya wanapaswa sasa kushikana mikono na kupiga kelele usoni mwa magaidi kwamba: "Je suis Bruxelles" - "Sote ni Brussels." "Hamtoweza kutunyamanzisha."

"Mungu mkubwa," alipiga kelele moja wa washambuliaji kwenye uwanja wa ndege Zaventem, kabla ya kuripua mkanda wake wa miripuko. Kuuwa katika jina la dini. Baada ya mashambulizi kadhaa mjini Paris, Istanbul na kwingineko, ipo haja ya kufanyakazi ya ziada kupambana na ugaidi. Magaidi wana uwezo wa kuuwa pasipo kuchaguwa, kusimamisha taifa zima na kusababisha machafuko.

Taifa laazima lijibu kwa nguvu zaidi kadiri iwezekanavyo. Iwapo wachunguzi na polisi wanahitaji zana zaidi, laazima wapatiwe. Ulinzi wa taarifa na haki za mtu laazima vichukuwe nafasi ya nyuma; kwa mfano, wakati wa kuchambua data za mawasiliano. Usalama wa wote uko hatarini.

Mwandishi wa DW mjini Brussels Bernd Riegert.
Mwandishi wa DW mjini Brussels Bernd Riegert.

Waziri mkuu wa Ubelgji Charles Michel alisema kwamba jibu letu linapswa kuwa "tulivu, la maana na kuonyesha mshikamano." Hilo ni sahihi, lakini mwishowe laazima kuwepo na jibu. Mashirika ya ujasusi barani Ulaya laazima yashirikiane vizuri. Watu wamekuwa wakijaribu kufanikisha hili kwa miaka sasa, lakini juhudi zao bado hazijapata mafanikio yanayotakiwa.

Kazi ya kijasusi inapaswa kuimarishwa, na uzuwiaji pia. Hatuwezi kuendelea kusimama na kuangalia wakati vijana waliojazwa itikadi kali kutoka Syria na Iraq wanarejea Ulaya na, maadam hawatendi uhalifu, wanaweza tu kuwekwa chini ya uangalizi hapa. Watu hao ambao ndiyo wanaunda makundi ya kigaidi barani Ulaya, wanapaswa kunyang'anywa uraia wao mara wanapofanza safari bila tiketi kurudi Ulaya.

Ili kufanikisha hili, ni muhimu kwa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya kulindwa vizuri zaidi. Hadi sasa hakuna ukaguzi wa kudumu kwa raia wa Ulaya wanaosafiri kwenda au kutoka Umoja wa Ulaya. Ukaguzi huu unapswa kuanzishwa haraka kuliko ilivyopangwa sasa. Mitandao ya kigaidi nchini Ubelgji iliweza kutanuka na kujiimarisha bila kizuizi kwa miaka kadhaa, na sasa hilo linasababisha athari chungu.

Lakini je, hali ni bora katika mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya mfano Ufaransa, Ujerumani? Mashambulizi ya uoga ya magaidi hao yanatufanya tubakie midomo wazi, wenye hasira, kwa sababu tunajihisi bila msaada. Nini tunaweza kufanya?

Mwandishi: Bernd Riegert/DW Brussels

Mfasiri: Iddi Ssessanga

Mhariri: Oummulkheir Hamidou