1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Kufutwa kesi ya Kenyatta ni pigo kwa haki

Abdu Said Mtullya5 Desemba 2014

Kesi ambayo ingelikuwa ya kwanza dhidi ya kiongozi wa nchi, aliemo madarakani, kwenye Mahakama ya Kamataifa , imesambaratika Kutokana na ukosefu wa ushahidi Mahakama hiyo imeamua kuifutilia mbali kesi hiyo.

https://p.dw.com/p/1DzvW

Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa Mahakama Kuu ya Kimataifa na kwa wapenda haki duniani kote. Mahakama hiyo iliundwa kwa lengo la kuikomesha tabia ya kutowaadhibu wanaotenda uhalifu dhidi ya ubinadamu . Nchi 122 ni wanachama wa Mahakama ya mjini the Hague. Kenya pia ilitia saini yake katika mkataba wa Rome ulioianzisha Mahakama ya mjini the Hague.

Andrea Schmidt
Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Andrea Schmidt.Picha: DW

Asasi za kiraia zataka hatua

Asasi nyingi za kiraia zilishiriki katika uasisi wa Mkataba huo wa Rome ambao ndiyo msingi wa Mahakama ya kimataifa kwa sababu asasi hizo hazikuweza tena kuvumilia kuona haki za binadamu zikikiukwa bila ya wahalifu kuchukuliwa hatua.

Mambo yalienda mrama tokea mwanzo kabisa. Mapema kabisa wakati wa kuitayarisha kesi, hiyo mahakimu walikuwa wamegawanyika. Kwa mfano hakimu wa kijerumani Hans-Peter Kaul aliefariki mnamo mwezi wa Juni aliipinga kesi hiyo kufanyika mjini The Hague na kuhoji kwamba uamuzi juu ya uhalifu uliotendeka ungeliweza kutolewa nchini Kenya.

Uchunguzi wa taabu uliofanywa na mwendesha mashtaka wa hapo awali Moreno Ocampo aliemtangalulia mwendesha mashtaka wa sasa Ben Souda, juu ya ghasia za mwaka 2008 zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya alfu moja na maalfu ya wakimbizi wa ndani-uchunguzi huo ulikabiliwa na vizingiti virefu sana.

Kadri muda ulivyokuwa unaenda ndivyo mashahidi walivyoendelea kujitoa,ama hawakuaminika au walitoweka bila ya kuacha alama yoyote. Hati muhimu zilichapishwa nusu nusu au hazikutolewa kabisa.

Kesi yaahirishwa mara kwa mara

Mnamo mwaka uliopita,kuanzishwa kwa kesi kuliahirishwa mara kwa mara.

Mashtaka yalikuwa juu ya kuhusika, lakini siyo moja kwa moja, na mauaji,kuwaandama na kuwatimua watu kutoka kwenye maakaazi yao kwa kutoa msaada wa fedha kwa watendaji uhalifu. Rais Kenyatta alikataa kuionyesha hadharani miamala yake ya fedha ingawa hapo awali aliahidi kushirikiana na mahakama.

Hata hivyo kwa Kenyatta na kwa washtakiwa wengine kwanza Mahakama ilipaswa kuthibitisha iwapo walikuwa na hatia.

Lakini kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu,wahanga na kwa ndugu wa watu walioathirika, nchini Kenya hiyo ilikuwa ishara ya maafa, kwamba kesi imesambaratika kutokana na ukosefu wa ushahidi.Watu hao walikuwa na haki kabisa ya kutumai kuona mahakama ikiubainisha ukweli hadharani na kutumia uwezo wake wote ili kuadhibu uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kazi iliyofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya mjini tha Hague hadi sasa ni finyu, kwani mpaka wakati huo mahakama hiyo imetoa hukumu tatu.

Mbili zilikuwa za kuwatia wahalifu hatiani, na moja ilikuwa ya kumwachia mshtakiwa baada ya kutopatikana na hatia. Jee Mahakama ya kimataifa ya mjini Tha Hague ni chui kibogoyo? Kwa kweli haipasi kuwa hivyo.Lazima kosoro zilizomo tokea mwanzo katika mahakama hiyo ziondolewe.Mahakama hiyo inapaswa iimarishwe vizuri, siyo kifedha tu bali pia katika muundo wake. Mahakama hiyo bado inategemea ushirikiano wa nchi zinazohusika na yale yaliyotukia. Utaratibu huo lazima ubadilishwe.Mahakama ya mjini The Hague inahitaji kuwa na polisi wake,watakaoweza kufanya uchunguzi bila ya kuingiliwa na kuweza kuwakama watuhumiwa.

Wachunguzi wanapaswa kuwa na fedha za kutosha ili kuweza kuwalinda mashahidi.Pia wanapaswa kuwa na uwezo wa kufanya uchunguzi katika sehemu husika bila ya kuwekewa mipaka.

Hakuna mbadala wa Mahakama ya Kimataiafa ya mjini The Hague.Tabia ya kutoawaadhibu wahalifu wa kivita,mauaji ya halaiki,chuki na uchochezi lazima ikomeshwe.

Wahanga na jamaa zao wanapaswa kuwa na uhakika kwamba mahakama ya kimataifa ni chombo huru,kinachoendesha kesi kwa njia ya haki na wahalifu wote wanawajibishwa bila ya kujali ngazi zao za kimajii.

Mwandishi:Andrea Schmidt.

Tafsiri:Mtullya abdu.

Mhariri:Yusuf Saumu