1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

umbukumbu ya unyenyekevu ya Steinmeier Yad Vashem

24 Januari 2020

Rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier ahutubia Yad Vashem nchini Israel katika kongamano la kimataifa dhidi ya chuki dhidi ya wayahudi kuadhimisha miaka 75 tangu kambi ya maangaamizi ya Auschwitz ilipokombolewa

https://p.dw.com/p/3Wkp0
Israel Jerusalem | 75. Jahrestag Befreiung von Auschwitz | World Holocaust Forum | Frank-Walter Steinmeier, Bundespräsident
Picha: Reuters/Pool/A. Sultan

"Huruma ya aina gani, jazza ya aina gani nnaweza kuzungumzia mbele yenu hii leo katika kumbusho hili la Yad Vashem" hivyo ndivyo rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier alivyoanza hotuba yake katika kongamano la kimataifa kuhusu mauwaji ya halaiki ya Wayahudi - World Holocaust Forum. Na kusema kweli halikuwa jambo la kawaida kwa rais wa shirikisho la jamahurin ya Ujerumani kuhutubia katika jengo muhimu la kumbukumbu za mauwaji ya halaiki ya wayahudi - Holocaust nchini Israel.

Yeye, mwakilishi wa ngazi ya juu kabisa wa nchi ya wenye hatia. Mtu ambae kizazi cha wazee wake na kile cha mabibi na mababu zake wamewauwa hadi mwaka 1945 wayahudi milioni sita.

Deutsche Welle Marcel Fürstenau Kommentarbild ohne Mikrofon
Mwandishi wa DW Marcel Fürstenau.Picha: DW

Miaka 75 baada ya kukombolewa kambi ya maangamizi ya Auschwitz, Steinmeier ameshukuria "mkono ulionyoshwa na manusura". Ameitaja kuwa ni "miujiza ya suluhu" ile hali kwamba wa Israel na ulimwengu kwa jumla wanaiamini upya Ujerumani. Maneno ya unyenyekevu ambayo hayana mfano. Steinmeier analinganisha makosa yasiyokuwa na mwisho ya Auschwitz na aibu inayozidi kupata nguvu inayoshuhudiwa wakati huu tulio nao.

Zimwi lile lile linachomoza

Kwa sababu hisia za chuki dhidi ya wayahudi nchini Ujerumani hazikuanza mwaka 2020 kudhihirika hadharani. Hajachelea kuzungumzia kuhusu "mazimwi waovu" wanaoeneza hisia za chuki dhidi ya wayahudi nyumbani. Ameitaja  njama iliyoshindwa ya kutaka kushambulia jumba la ibada la wayahudi mjini Halle an der Saale mnamo siku ambayo wayahudi walikuwa wakisherehekea siku kuu yao muhimu ya Yom Kippur.

Fasaha ya rais wa shirikisho haikuwa na mfano."Sio wale wale. Lakini zimwi ni lile lile alisema"

Kumbusho la mauwaji ya halaiki ya Holocaust la Yad Vashem bila ya shaka ni mahala penyewe hasa kwa Steinmeier kuomba toba. Hisia ambazo huenda zikamzidi tena atakapozuru eneo lenyewe hasa la uhalifu dhidi ya ubinaadam -Auschwitz jumatatu inayokuja siku ambapo kambi hiyo ya mateso na maangamizi ilikombolewa.