1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mustakabali wa mashaka kwa serikali ya Merkel

Iddi Ssessanga
27 Mei 2019

Nchini Ujerumani, alau vyama rafiki na Umoja wa Ulaya ndiyo washindi katika uchaguzi. Hata hivyo kushindwa kwa SPD kunaiweka hatarini serikali ya kansela Merkel, anasema mhariri mkuu wa DW Ines Pohl katika uhariri wake.

https://p.dw.com/p/3J9Rb
Deutschland | Koalitionsgipfel im Kanzleramt | Andrea Nahles und Angela Merkel
Picha: picture-alliance/dpa/Bildfunkk/B. v. Jutrczenka

Hofu ilikuwa kwamba vyama vinavyoupinga Umoja wa Ulaya vingeibuka na ushindi katika uchaguzi wa Ulaya. Nchini Ujerumani, Austria na Uholanzi, angalau hilo halijatokea. Hayo ndiyo matokeo chanya ya uchaguzi wa mwishoni mwa wiki.

Mgawanyiko kati ya wazalendo na waungaji mkono wa Ulaya bila shaka uliwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura, ambapo mataifa mengi yameripoti idadi kubwa ya washiriki kuliko kawaida.

Pia, watu zaidi wenye umri wa chini ya miaka 30 wamepiga kura mwaka huu kuliko ilivyokuwa katika miaka ya nyuma - ushahidi zaidi kwamba wanaguswa na mada ya Ulaya na suala la namna tunavyotakwa kuishi pamoja.

Katika tabaka hili la umri, washindi wa wazi ni vyama vya watetzi wa mazingira - yaani Kijani, ambao waliweza kulielezea kwa ufasaha, suala la wakati ujao - kuhusu ulinzi wa mazingira - kwa faida yao.

Ines Pohl
Mhariri Mkuu wa DW Ines PohlPicha: DW/P. Böll

Janga kwa chama cha SPD

Kwa chama cha Social Democratic cha Ujerumani hata hivyo, Jumapili imekuwa janga kubwa. Chama hicho kikongwe zaidi cha kidemokrasia nchini Ujerumani kimeshuka chini ya asilimia 16 katika ya Ulaya.

Na si hivyo tu: Uchaguzi wa serikali za miji ulifanyika pia hiyo Jumapili katika jimbo la Bremen, jimbo la shirikisho ambalo chama hicho kimelitawala kwa miaka 73. Si hivyo tena. Mshindi wa uchaguzi huo ni mgombea wa chama cha CDU kwa mara ya kwanza kabisaa.

Vipigo hivi viwili havitapita bila madhara. Ni dhahiri kwamba chama hicho kinakabiria kuanguka kabisaa, na kujijenga upya ndiyo njia pekee kitakuwa na nafasi ya kuwa na mustakabali mwema.

Uchaguzi wa mapema unawezekana

Kutakuwa na hoja mjini Brussels katika siku zijazo kuhusu chama gani kitapata kujaza nafasi ipi miongoni mwa nafasi za juu. Nchini Ujerumani, utakuwa na msingi zaidi. Swali kuu linaweza kuwa: Ni kwa muda gani zaidi muungano huu tawala unanuwia kuendelea kujitesa wenyewe na taifa kwa ujumla?

Baada ya wikendi hii, inawezekana kabisaa kwamba, baada ya miaka 14, enzi ya Merkel itafikishwa mwisho na chama mshirika katika muungano - SPD - na kutakuwa na uchaguzi wa mapema baadae mwaka huu. Utakuwa uchaguzi wenye maswali mengi ya wazi, na uhakika mmoja: Angela Merkel hatogombea tena.

Mwandishi: Ines Pohl

Tafsiri: Iddi sessanga

Mhariri: Sylvia Mwehozi