1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushawishi wa Ujerumani iliyoungana

2 Oktoba 2015

Ujerumani iliyoungana inatimiza miaka 25. Katika miaka hii 25 watu wa upande wa mashariki na magharibi wamekuwa pamoja, hata hivyo katika maeneo mengi kumekuwa na tofauti na bado hawajakuwa wamoja, ni wageni.

https://p.dw.com/p/1GhaF
Deutschland Mauerfall Grenzöffnung Berliner Mauer mit dem Brandenburger Tor
Ummati wa watu katika eneo maarufu la Brandenburg mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Wajerumani wanailalamikia hali hii, lakini hii ni kawaida ya Wajerumani. Tofauti nchini Ujerumani , kati ya kusini na magharibi, kati ya kaskazini na mashariki ni hali ya kawaida kabisa katika historia ya nchi hii.

Serikali kuu kama ilivyo katika nchi jirani ya Ufaransa , inaeleweka, lakini kwa Ujerumani ni kitu tofauti kabisa. Ujerumani wakati wote ni mkusanyiko wa majimbo, ambayo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa.

Umoja katika Ujerumani baada ya robo karne ya maajabu ya kisiasa. Ni nchi inayopendwa. Ni nchi inayojulikana sana. Ni nchi muhimu. Ni nchi iliyo na nguvu kubwa ya kiuchumi. Ikiwa na mfumo wa kijamii unaovutia duniani . Ni nchi ambayo haijigambi kwa nguvu za kijeshi , ama silaha nzito, badala yake inatumia diplomasia, ikionesha kujizuwia , kuonesha uwezo wa kushawishi tu.

Ni jamhuri ya watu, kinyume na ilivyokuwa hapo nyuma, ambapo iliwatisha majirani na baadaye dunia kwa juma.

Dunia inaiangalia Ujerumani

Kwa upande wa Ujerumani, hususan Angela Merkel , dunia inamuangalia. Hata bila ya kuwa mwanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa , ushauri wa Ujerumani na kansela una uzito mkubwa. Katika bara la Ulaya pia na duniani kwa jumla.

Kwa tahadhari kabisa, hali hii ya nguvu kubwa, ni uwezo mkubwa wa kisiasa na kiuchumi na bila shaka ni moja kati ya nchi tano zenye ushawishi mkubwa duniani. Lakini pamoja na hayo ni nchi isiyojiamini. Inakosa kujiamini binafsi.

Kwasababu kwa jukumu lake hilo jipya, na matarajio , yaliyowekwa kwa Wajerumani , huenda yakaleta matokeo mabaya.

Alexander Kudascheff
Mwandishi wa maoni haya: Alexander KudascheffPicha: DW

Jukumu la Ujerumani

Ujerumani inatambua kwamba inapaswa kuchukua jukumu kubwa zaidi, kuliko inavyofanya. Lakini kwa undani kabisa, licha ya kuungwa mkono na wananchi wake wengi, inasita. Ujerumani inataka kuchukua msimamo wa kati kwa kati.

Ujerumani kisiasa imejikita upande wa magharibi. Siasa za hapo kabla za kuyumba yumba haziko tena. Lakini pia jamhuri ya Ujerumani inabadilika badilika ; baina ya mtazamo imara wa kisiasa wa nadharia za vitendo na kile kinachoonekana kuwa ni hali ya kutofikia kupindukia hali hii inayovutia hadi kufikia kufurahia maisha kupindukia na kujikuta katika hali ya kutoweza kutabirika.

Binafsi kansela Merkel ambaye amejingea umaarufu wa kutumia zaidi busara, hayuko huru. Kwa upande mmoja ametangaza mabadiliko ya vyanzo vya uzalishaji nishati kwa kufunga vinu vya kinyuklia kutokana na ajali iliyotokea Fukushima nchini Japan, bila kuangalia gharama za hatua hiyo.

Kwa upande mwingine katumbukia katika mzozo wa wakimbizi , kwa kutupilia mbali sheria zote kutokana na misingi ya ubinadamu , na kufungua mipaka, kwa mshangao mkubwa wa majirani zake wa Ulaya.

Anajikuta kwa mshangao , katika hali ya "ubeberu wa kiutu."

Mwandishi: Kudascheff, Alexander / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Yusuf Saumu