1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Ulaya imo katika wasiwasi mkubwa

Zainab Aziz
10 Novemba 2016

Hatukijui kile tunachoweza kutarajia kutoka kwa Donald Trump, Baada ya kuchaguliwa kwake, ni rahisi kudhania kuwa mambo yatakuwa mabaya zaidi, kwa sababu mengi kati ya aliyoyatamka yanaweza kuathiri maslahi ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/2SSnw
US-Präsidentschaftswahl 2016 - Sieg & Rede Donald Trump
Picha: Reuters/C. Allegri

Trump amedhihirisha shaka yake juu ya jumuiya ya kujihami ya NATO, ameeleza hisia zake juu ya kumpenda Putin, ametoa maneno ya kibaguzi kwa wahamiaji na anataka kuifutilia mbali mikataba ya biashara - orodha ya malalamiko ni ndefu na ni ya kutisha. Hakuna ajuwae hasa katika haya yote ni yepi ambayo atayatekeleza katika sera yake ya kisiasa ambayo imechanganyikiwa au yupi kati ya wafuasi wake atakefuata mawazo sawa na yake. Ukweli huu unatia wasiwasi.

Ni hatari sana pia. Marekani imewahi kuwa na marais ambao hawakuwa na umarufu mkubwa, lakini hakuna mtu aliyewahi kuwatia hofu washirika kama Donald Trump

Matokeo ya uchaguzi yanaleta hisia kana kwamba Enzi imefikia mwisho. Enzi juu ya mahusiano kati ya Marekani na nchi za Ulaya ambayo kwa uwezo wake wote pamoja na udhaifu wake yalikuwa ni mahusiano yaliyoleta utulivu katika siasa za dunia. Iwapo Trump ataendeleza shauku yake ya kujitenga, basi biashara ya kimataifa itakumbwa na dhoruba. Ushirikiano wa Usalama ulioilinda Ulaya kwa miongo kadhaa  unaweza kuvunjika. Na kama Trump na Putin watakaribiana, basi nguvu katika mfumo wa siasa za dunia zitabadilika.

Kama tunavyojua kupanda kisiasa kwa Donald Trump kunaweza kuleta athari kubwa au kusababisha mwisho wa demokrasia huria. Trump anaweza kuwa kichocheo cha kuongezeka siasa za mrengo wa kulia zinazopendwa na wanaharakati  wa Ulaya.

Chukulia mfano wa Recep Erdogan wa Uturuki, Vladimir Putin wa Urusi, au serikali yenye mtazamo mkali ya Korea ya Kaskazini na pia mtawala wa Philippine Rodrigo Duterte, yote haya yanasabisha hofu katika mazingira ya siasa za kimataifa.

USA Washington Anti-Trump Protest Wahlnacht
Bango la kumkashifu TrumpPicha: picture-alliances/dpa/M. Reynolds

Kwaheri Marekani!

Hata kama ingewezekana kuepuka mazingira mabaya ya kisiasa au mshtuko ambao uliosababishwa na kampeni hii umekwenda kwa kina kirefu.

Huu ni mwisho wa ndoto ya Marekani, hadithi ya Bob Dylan na Susan Sontag, Robert Redford na mashujaa wengine. Wote hawa walikuwa wamezikwa chini ya matamshi ya chuki ya Donald Trump, ambayo yalivunja miiko yote kama ubaguzi wa kijinsia, ubaguzi wa rangi, uongo na hasira yake.

Ni wakati wa kusema kwaheri kwa Marekani tuliyoijua na kuipenda.

Dunia imekuwa mahali pa hatari zaidi na wala haitabiriki. Donald Trump anaweza kuwa chanzo cha hofu yetu.

Kuna matumaini kidogo kwamba sisi tutaepukana na hali mbaya zaidi. Lakini kwa Trump tunaweza kurudi tena nyuma katika nyakati za giza.

 

Mwandishi. Zainab aziz/Babra Wesel

Mhariri Iddi Ssessanga