1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya chama cha mrengo mkali wa kulia NPD

Abdu Said Mtullya3 Desemba 2013

Wahariri wanazungumzia juu ya hatua ya kuwasilishwa mbele ya Mahakama Kuu ya katiba ya Ujerumani, kwa maombi juu ya kukipiga marufuku chama cha mrengo mkali wa kulia,NPD

https://p.dw.com/p/1ASTZ
Maandamano dhidi ya chama cha mrengo mkali wa kulia NPD
Maandamano dhidi ya Chama cha mrengo mkali wa kulia NPD.Picha: picture-alliance/dpa

Chama cha NPD pia kina siasa za kibaguzi na kinazingatiwa kuwa ni tishio kwa demokrasia nchini Ujerumani. Maombi kwenye Mahakama Kuu ya katiba yamewasilishwa na Baraza la wawakilishi wa majimbo yote 16 ya Ujerumani, yaani tawi la juu la Bunge la Ujerumani.

Mhariri wa gazeti la "Donaukurier" anakumbusha katika maoni yake kwamba juhudi za kukipiga marufuku chama cha NPD zilishindikana miaka 10 iliyopita baada kugundilika kwamba makachero wa serikali walijipenyeza katika uongozi wa chama hicho.

Mhariri wa "Thüringische Landeszeitung" anasema kupigwa marufuku kwa chama hicho hakutakuwa na maana ya kutoweka kwa itikadi zake. Naye mhariri wa gazeti la "Münchner Merkur"anasema katika maoni yake kwamba lingekuwa jambo zuri sana na la kushangiiwa endapo chama hiyo cha siasa za mrengo mkali wa kulia kingelipigwa marufuku. Lakini jambo moja linapaswa kuliangaliwa kwa makini sana kwamba kesi dhidi chama hicho inaweza kugeuka na kuwa kama tangazo la biashara kwa chama hicho.

Gazeti la "Rhein-Necker"linatanabahisha kwamba kuifikisha kesi mahakamani dhidi ya chama cha NPD hakuna maana ya uhakika wa kufanikiwa. Hatahivyo viongozi wa Ujerumani hawapaswi kusubiri mpaka chama hicho cha kifashisti mamboleo kichukue mamlaka ya nchi. Mtungi utakuwa umeshapasuka!

Machozi ya mamba kwa ajili ya wakimbizi

Gazeti la "Straubinger Tagblatt linatoa maoni juu ya hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya ya kuanzisha mtandao wa kuilinda mipaka ya Ulaya ili kuyaokoa maisha ya wakimbizi. Gazeti hilo linasema kuwa Umoja wa Ulaya unahubiri haki za binadamu lakini wakati huo huo unachukua hatua kali dhidi ya wahamiaji .Ni sawa kufanya hivyo lakini ukali huo uelelekezwe kwa,wahalifu wanaofanya biashara ya kuwauza binadamu.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Yusuf Saumu