1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatari ya saratani

27 Oktoba 2015

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanatoa maoni juu ya vyakula vinavyoweza kusababisha saratani, na juu ya matokeo ya uchaguzi wa nchini Poland

https://p.dw.com/p/1Gum6
Picha: Imago/Science Photo Library

Gazeti la "Donaukurier" linazungumzia juu ya ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO juu ya vyakula vinavyoweza kusababisha maradhi ya saratani. Shirika hilo limesema katika ripoti yake kwamba nyama iliyosindikwa kama vile ya nguruwe na soseji zinaweza kusababisha saratani utumboni.

Mhariri wa gazeti la"Donaukurier" anawataka watu wasikubali kuingiwa na kiherehere juu ya ripoti hiyo.

Mhariri huyo anasema mashirika mengine ya kimataifa yanoyoshughulikia utafiti wa maradhi ya kansa yameeleza kwamba pana ni ushahidi kidogo tu unaoweza kuthibitisha kwamba binadamu anaweza kupatwa na maradhi ya kansa ikiwa anakula nyama nyekundunyekundu. Gazeti la "Donaukurier" linatilia maanani kwamba katika nchi fulani nyama inaliwa sana lakini kiwango cha watu kupatwa na ugonjwa wa saratani ni cha chini.

Lishe bora bila ya nyama

Mhariri wa "Mitteldeutsche" anasema binadamu anaweza kupata lishe ya afya bila ya nyama.Lakini haina maana kwamba mtu aache kila kitu. Ripoti ya Shirika la Afya Duniani, imetoa hoja tunazopaswa kuzitilia maanani.Hata hivo ripoti haionyeshi kila kitu juu ya mwambatano uliopo kati ya ulaji wa nyama na maradhi ya kansa.Ndio kusema hakuna haja ya kuwa na kiherehere .Lakini mhariri wa gazeti la "Mitteldeutsche" anawataka watu wazingatie ushauri wa wataalamu.

Mhariri wa gazeti la "Ludwigsburger Kreiszeitung" anasema yapo mambo mengi yasiyojulikana juu ya gharama zinazotokana na mgogoro wa wakimbizi.Mhariri huyo anasema hakuna mtu anaejua kwa uhakika ni wakimbizi wangapi watakaokuja barani Ulaya. Mhariri wa gazeti hilo anatumai kwamba bara la Ulaya litafanikiwa kuuweka utaratibu mzuri wa kugawana jukumu la kuwashughulikia wakimbizi.

Mhariri huyo pia anatumai kwamba nchi za Ulaya zitaweza kuung'oa mzizi unaosababisha ukimbizi kabla ya kutoa miito ya kutenga kiasi kikubwa cha fedha kitakachowagharimu walipa kodi, hali itakaowapa kichwa watu wenye itikadi kali kama wa kundi la Pegida. Mhariri wa gazeti la "Landeszeitung" anazungumzia juu ya mabadiliko ya serikali nchini Poland.

Anasema mabadiliko hayo yaliyotokea baada ya kufanyika uchaguzi, ni suala tunalopaswa kulitilia maanani. Mhariri huyo anaeleza kuwa serikali za mrengo wa kulia zinachaguliwa katika nchi za Ulaya Mashariki na kaskazini, wakati kusini mwa Ulaya zinazochaguliwa ni serikali za mrengo wa kushoto.

Wakimbizi waendelea kuwasili
Wakimbizi waendelea kuwasiliPicha: picture-alliance/dpa/AA/C. Genco

Gazeti la "Landeszeitung" linatahadharisha kwamba bara la Ulaya linagawanyika. Gazeti hilo linasema mgawanyiko huo unautikisa msingi wa sera ya bara la Ulaya-yaani utayarifu wa kufikia mwafaka. Mhariri wa gazeti la "Landeszeitung anasisitiza kuwa ni muhimu kwamba Ujerumani na Ufaransa zimeelewana tena juu ya suala la wakimbizi.

Ujerumani na Ufaransa zinapaswa kuongoza katika bara linalosonga mbele katika njia mbili zinazoekelea kwenye upande mmoja.

Mwandishi:Mtullya Abdu. Deutsche Zeitungen

Mhariri:Josephat Charo