1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya mkutano wa NATO

Abdu Said Mtullya2 Aprili 2014

Wahariri wanatoa maoni juu ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Nato na pia juu ya uhusiano baina ya Nato na Urusi kwa jumla

https://p.dw.com/p/1Ba4R
Mawaziri wa NATO wakutana mjini Brussels
Mawaziri wa NATO wakutana mjini BrusselsPicha: Getty Images/Afp/John Thys

Gazeti la "Der Tagespiegel" linazungumzia juu ya mkutano wa mawaziri wa Nato uliofanyika jana mjini Brussels. Mhariri wa gazeti hilo anasema mkutano huo umeonyesha kwamba katika kuikabili Urusi njia zote za kisiasa,kidiplomasia na kijeshi zinapaswa kuzingatiwa.

Mhariri huyo anatilia maanani kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za NATO wameeleza wazi ,kuwa ikiwa Urusi itaendelea na shughuli za kujitandaza nchi za NATO zitaweka ulinzi wa kijeshi karibu na mipaka ya Urusi.

Mhariri wa gazeti la "Rhein" anazungumzia juu ya uhusiano wa nchi za Nato na Urusi kwa jumla, na anaeleza.kwamba mgogoro mkubwa utatokea baina ya nchi za magharibi na Urusi, ikiwa Ukraine, Georgia Moldova na Azebaijan zitainizwa katika Nato. Katika miaka ya nyuma ,mpango huo uliwekwa kando ili kuepusha mvutano na Urusi.

Hata hivyo ikiwa viongozi wa Urusi wataendelea kuukataa mkono wa amani na badala yake kuendelea na nyendo kama zile za jimbo la Krimea, basi vita baridi hakika vitarejea. Mawaziri wa Nato hawakuazimia chochote kwenye mkutano wao wa jana , lakini wametamka wazi kwamba jumuiya yao haitasimama kando, mikono kiunoni wakati Urusi inaendelea kujitandaza.

Haja ya kujiunga na NATO

Gazeti la"Volsstimme" linasema mgogoro wa Ukraine umeonyesha kwa nini baadhi ya nchi za Ulaya ya Mashariki zimejiunga na mfungamano wa kijeshi wa NATO. Hata hivyo mhariri wa gazeti hilo ameyanukuu maneno ya busara ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier, aliesema wazi kwamba ,kwa sasa Ukraine haitaingizwa katika NATO.

Na gazeti la "Nürnberger Nachrichten" limebainisha jambo moja muhimu ,kwamba licha ya mgogoro wa Ukraine kuwa mzito kutokana na Urusi kulimega jimbo la Krimea kutoka Ukraine, nchi za magharibi na Urusi hazitarejea katika enzi za vita baridi. Gazeti la "Eisenacher Presse" linazishauri nchi za magharibi kuepuka kutumia misuli katika kuutatua mgogoro uliopo.

Linasema inapasa kuyatekeleza yaliyokubaliwa mnamo miaka ya 90 kwamba majeshi ya nchi nyingine za Nato yasiwekwe katika nchi kama Poland au nchi nyingine za Ulaya ya mashariki. Nchi za Nato zinapaswa kuyazingatia makubaliano, siyo kwa sababu ya kuiogpoa Urusi, bali kwa sababu inapaswa kuweka kipa umbele katika suluhisho la amani.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Yusuf Saumu