1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

Abdu Said Mtullya13 Mei 2009

Wahariri wasema lazima haki itendeke.

https://p.dw.com/p/HpAD
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 ziarani Mashariki ya Kati.Picha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya mtuhumiwa wa mauaji ya wayahudi alfu 29, na kwa mara nyingine juu ya ziara ya Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 katika mashariki ya kati.

Juu ya mtuhumiwa wa mauaji ya wayahudi, John Demnjanjuk gazeti la Niedersächsiche Allgemeine linasema kinachohitajika ni kutendeteka haki kwa niaba ya wahanga wa udhalimu, ambapo Ujerumani bado ina wajibu, hata ikiwa leo nchi hii inaongozwa katika misingi ya kisheria. Gazeti linasema Ujerumani ina wajibu wa kisiasa na kimaadili, na hiyo ina maana kwamba, hata leo, kinachopaswa kufuatiliwa kisheria lazima kifuatiliwe .


Mhariri wa gazeti la Der neue Tag anatilia maani kwamba Demnjanjuk ni mzee na mgonjwa na yumkini hataweza kuhilimi harubu za jela. Lakini mhariri huyo anafafanu kuwa labda hali yake dhaifu inaweza kuhalalisha moyo wa huruma, ambao yeye mwenyewe hakuwa nao. Lakini katika kuwa na moyo huo wa huruma inapasa kutilia maanani kwamba Demnjanjuk alitumia nguvu za ujana wake, kuwasukumia maalfu ya watu, wazee, watoto na wanawake katika vizimba vya gesi.

Na gazeti la Badische Neueste Nachrichten linasema , haidhuru kitu jinsi kesi ya Demnjanjuk itakavyoamuliwa, muhimu ni kwamba kesi hiyo ni onyo.

Na kwa mara nyingine baadhi ya wahariri wa magazeti leo wameandika juu ya ziara ya Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 katika mashariki ya kati ambayo kwa kiasi fulani imegubikwa na utatanishi.

Hatahiyvo gazeti la Augsburger Allgemeine linasema kwamba baba Mtakatifu amegusa mioyo ya watu wengi nchini Israel licha ya kuwapo hisia za chini chini juu ya kumwambatanisha kiongozi huyo wa kanisa katoliki na uhalifu uliotendwa na utawala wa Hitler.Lakini gazeti la Münchner Merkur linanasihi kwa kusema,kuwa Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 angelisisitiza tena, msimamo wa baba mtakatifu aliemtangulia, John Paul wa pili aliekwenda kwenye ukuta wa kilio mjini Jerusalem na kuomba dua la kuleta maridhiano. Mhariri wa Münchner Merkur anasema, hasa kwa kuwa Benedikt wa 16 mwenyewe ni mjerumani, angelipaswa kutoa ishara thabiti ya maridhiano kwa niaba ya kanisa katoliki na kwa niaba ya umma wa Ujerumani.

Mwandishi /Abdul Mtullya.

Mhariri/M.Abdul-Rahman