1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri

8 Januari 2008

Wahariri watoa maoni yao juu ya kampeni za uchaguzi wa majimbo.

https://p.dw.com/p/CmQe


Wakati uchaguzi wa majimbo unakaribia kufanyika nchini Ujerumani vyama vilivyomo katika serikali ya mseto vinatupiana makombora ya kapakana matope.

Wanasiasa wa vyama vilivyomo katika serikali ya mseto yaani chama cha Social Demokratik , CDU na CSU wanalaumiana na kupakana matope sasa wakati ambapo wajerumani kwa mara nyingine wanajitayarisha kupiga kura katika uchaguzi wa majimbo.

Wahariri wa magazeti wameweza kutambua kwamba kauli za kulaumiana miongoni mwa wanasiasa wa vyama vikuu hapa nchini Ujerumani ni sehemu ya kampeni ya kujijengea umaarufu miongoni mwa wastahiki wakati wa kupiga kura.

Masuala mawili yamejitokeza katika kampeni hiyo ya propaganda.

Kwanza ni mapendekezo juu ya kukabiliana kwa ufanisi na uhalifu wa vijana na pili ni juu ya mshahara wa kima cha chini.

Juu ya hayo Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linauliza jee vita hivyo vya propaganda vitaendelea hadi lini.? Lakini zaidi hasa, mhariri wa gazeti hilo ana wasi wasi mkubwa kutokana na jinsi wanasiasa hao wanavyoraruana kwa kauli.

Mhariri anasema katika maoni yake kwamba wanasiasa wa vyama vilivyomo katika serikali ya mseto wanakabiliana kwa maneno ya mvutano kiasi kwamba inakuwa vigumu kuamini kuwa baada ya hapo wataweza kutazama ana kwa ana na kuendelea na kazi za uongozi wa serikali.!

Hayo pia anasema mhariri wa gazeti la OSTSEE-kutoka mji wa Rostock mashariki mwa Ujerumani.

Mhariri huyo anasema kilichoanza kama kampeni za uchaguzi wa majimbo sasa kimegeuka kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa katika ngazi ya shirikisho.
Mhariri huyo anakumbusha mkasa uliotokea hivi karibuni kwenye kituo cha treni mjini Munic ambapo mtu mmoja alivamiwa na vijana.

Gazeti linasema mkasa huo umekuwa nongwa, kwani unatamalaki mijadala yote ya kisiasa nchini.

Wanasiasa wa vyama vilivyomo katika serikali ya mseto wanautumia mkasa huo kana kwamba makombora ya kauli yatatatua tatizo la matumizi ya nguvu miongoni mwa vijana.

Gazeti jingine linalozungumzia mjadala huo linatoka mji wa LÜBECK. Na katika maoni yake mhariri wa gazeti hilo anasema , kama uhodari wa kuendesha kampeni , ni kutoa ahadi ambazo mtu hawezi kutimiza, basi uhodari huo upo katika jimbo la Hesse.

Gazeti hilo linaloitwa LÜBECKER NACHRICHTEN linatilia maanani kwamba wanasiasaa wa jimbo hilo la Hessen wanashikana makoo juu ya masuala ambayo asilani hayataamuliwa katika bunge la jimbo lao.

Wakati mjumbe wa chama cha CDU anatoa mapendekezo juu ya kuimarisha sheria dhihi ya vijana wahalifu, mshindani wake kutoka chama cha Social Demokratik anakusanya saini za kuunga mkono pendekezo la kuanzisha utaratibu wa mshahara wa kima cha chini Ujerumani kote.

AM.