1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAONI YA WAHARIRI

Mtullya, Abdu Said14 Februari 2008

Wahariri wa magazeti waunga mkono uamuzi wa Mahakama ya katiba.

https://p.dw.com/p/D7Pw


►◄

Maoni ya wahariri.

Katika maoni yao leo wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya uamuzi wa mahakama ya katiba kukataa kutumika utaratibu wa asilimia tano katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye jimbo la Schleswig-Holstein.


Katika ngazi ya majimbo na ya kitaifa, nchini Ujerumani kila chama lazima kipate asilimia 5 ya kura ili kuweza kuingia bungeni .

Lakini mahakama kuu ya katiba mjini Karlsruhe imepinga utaratibu huo kutumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye jimbo hilo la Schleswig-Holstein kaskazini mwa Ujerumani.

Mahakama imesema kihunzi hicho kinakiuka haki ya usawa kwa vyama vyote.

Katika maoni yao leo wahariri karibu wote wanaunga mkono uamuzi huo.
Gazeti la HANDELSBLATT linasisitiza mtazamo wake kuunga mkono uamuzi wa mahakama kwa kusema kuwa lengo la uchaguzi ni kutoa fursa sawa kwa vyama vyote

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ndio hasa unaotoa fursa hiyo- kwani mabunge yanatakiwa yawe na uwezo wa kutenda kazi kwa kujenga uwingi katika uwakilishi.

Gazeti linasema kuondolewa kipingele hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutaimarisha ushindani wa kisiasa.

Gazeti la GENERAL-ANZEIGER pia linaunga mkono uamuzi wa mahakama ya katiba, japo linatahadharisha kuwa jumuiya zenye itikadi kali pia zinaweza kuingia mabungeni.

Mhariri anasema, kwa kweli halitakuwa jambo la kufurahisha,ikiwa vyama vya mlengo wa kifashisti mamboleo navyo pia vitaingia katika bunge lakini pia inafaa kutambua kwamba,ikiwa kihunzi cha asilimia tano kitatumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa, jumuiya nyingine za wananachi adilifu pia zinaweza kuwa kando kutokana na kushindwa kupata asilimia tano ya kura. Kwa hiyo kwa jumla tunaweza kusema kuwa uamuzi wa mahakama ni nyongeza ya demokrasia.

Katika maoni yake Gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN linatilia maanani maslahi yanayowakilishwa na jumuiya ndogo ndogo.Jumuiya ambazo zisingeliweza kuvuka kihunzi cha asilimia tano.

Jumuiya ama vyama hivyo haviwezi kushindana na vyama vikuu.Ni kutoka na hayo kwamba uamuzi wa makahama kuu ya katiba mjini Karlsruhe ni wa haki.