1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Mtullya, Abdu Said10 Juni 2008

Magazeti ya Ujerumani leo yanatoa maoni juu ya ziara ya rais G.W.Bush barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/EGsM
Rais G.W. Bush akiwasili nchini Slovania na kupokewa na waziri mkuu wa nchi hiyo .Picha: AP

Magazeti ya Ujerumani leo yanazungumzia juu ya ziara ya rais G.W .Bush wa Marekani barani Ulaya na juu ya tofauti za mishahara baina ya wanawake na wanaume nchini Ujerumani.

Na gazeti la Financial Times Deutschland linazungumzia juu ya tishio kubwa la kuongezeka bei ya gesi hapa nchini.

Juu ya ziara ya rais Bush barani Ulaya mhariri wa gazeti linaloitwa Emder,anasema rais huyo atafanya ziara Ujerumani, lakini hakuna mtu mwenye hamu naye . Gazeti hilo linasema mtu anapata hisia, kwamba wenyeji wake wangependelea kuona itifaki zote zikienda haraka ,na ziara ikimalizika. Gazeti linaeleza kuwa hakuna rais wa Marekani aliewafanya watu watikise vichwa, kutokana na siasa zake, kama G.W .Bush.

Gazeti la Morgen Post pia limeandika juu ya rais Bush na wajerumani.

Gazeti hilo linasema ,katika macho ya wajerumani, Marekani imepetoza wajihi kwa kiwango cha kutisha. Mhariri wa Morgen Post anaeleza kuwa, kauli za ushari ambazo rais huyo amekua anataoa zimemfanya awe bwana hapendeki kwa wajerumani. Ni asilimia 30 tu ya wananchi wa Ujerumani ambao bado wana fikira nzuri juu ya Marekani. Gazeti linasema watu nchini Ujerumani sasa wana matumaini, kwamba mambo yatabadilika, atakapoingia rais mpya nchini Marekani.


Kuhusu masuala ya ndani magazeti yameandika juu ya tofuti za mishahara baina ya wanawake na wanaume na juu ya bei ya nishati ya gesi.


Gazeti la Mitteldeutsche Zeitung linatilia maanani kwamba kwa wastani mishahara ya wanawake ipo chini ya mishahara ya wanaume kwa asilimia 22 nchini Ujerumani. Gazeti linaeleza kuwa , sababu ya tofauti hiyo ni kwamba wanawake wanalazima,aghalabu kufanya mapumziko kutokana na uzazi. Muda unapotea. Kwa hiyo hawawezi kushindana na wanaume inapohusu muda wa kuwapo kazini. Lakini gazeti linauliza jee, jamii itapima hadhi ya mwanamke kutokana na mchango wake kazini, au kutokana na mchango wake katika jamii kwa ujumla

Gazeti la Financial Times Deutschland linazingatia tishio la mfumuko wa bei ya gesi nchini Ujerumani.

Gazeti hilo linashauri kuwa njia pekee ni kuimarisha ushindani ili wauzaji wa gesi wasiweze kuongeza bei jinsi wapendavyo.