1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

Abdu Said Mtullya6 Mei 2009

Wahariri wanasema Uturuki bado ina haki ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/Hkgi
Waturuki bado wana haki ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.Picha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya udhalimu uliotendeka katika Ujerumani Mashariki na juu ya mauaji yaliyotokea kwenye sherehe ya uchumba nchini uturuki.

Kadhalika wanafafanua msimamo wa mawaziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani kuhusu wafungwa wa jela ya Guantanamo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel jana alikitembelea kituo ambacho sasa kimekuwa kumbukumbu ya ukatili uliofanywa na idara ya usalama ya Ujerumani mashariki,iliyokuwa inaitwa Stasi.

Kituo hicho kilichotumika kama mahabusu kipo mjini Berlin. Wapinzani wa serikali walifungwa katika jela hiyo.

Juu ya ziara ya Kansela Angela Merkel kwenye kituo hicho gazeti la Nordkurier linasema, hiyo ni sehemu ya historia ya Ujerumani isiyopasa kusahauliwa.

Na mhariri wa gazeti la Cellesche Zeitung anasema wale wenye jitimae juu ya Ujerumani Mashariki ya zamani wajaribu kuzungumza na watu waliowahi kufungwa katika jela hiyo.


Kansela Angela Merkel alifanya ziara kwenye kumbukumbu ya udhalimu wa idara ya upelelezi ya ujerumani mashariki kama sehemu ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuondolewa kuta la Berlin.

Gazeti la Neue Tag linazungumzia juu ya mauaji yaliyotokea kwenye sherehe za uchumba nchini Uturuki.

Watu waliokuwa na silaha waliwashambulia jamaa waliokuwa wanasherehekea ghafla ya kuchumbiana. Katika shambulio hilo watu 44 waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa. Juu ya tukio hilo mhariri wa gazeti la Der neue Tag anasema mauaji hayo yasitumike kama sababu katika kuamua iwapo Uturuki iwe mwanachama wa Umoja wa Ulaya au la.

Kwa sababu wapo wale wanaotaka kutumia tukio hilo ili kujaribu kuonesha kwamba Uturuki bado haijafikia kiwango cha kupata uanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mhariri huyo anatilia maanani mauaji yaliyotokea nchini Ujerumani na ufidhuli wa mtu kama Josef Fritzl aliezaa na binti yake.

Gazeti la Landeszeitung Lüneburg pia linasema katika maoni yake kwamba mauji yaliyotokea kwenye sherehe za uchumba nchini Uturuki yasiwe mwao wa kisiasa katika kuamua juu ya kuipa au kuinyima Uturuki uanachama wa Umoja wa Ulaya. Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha juu ya isimu ya mwanadamu mwenyewe. Anasema nchini Ujerumani mauaji pia yanatokea. Hivyo basi, kuikatalia Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya ati kwa sababu ya mauaji yaliyotokea kwenye ghafla ya uchumba, litakuwa kosa.