1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano baina ya India na Pakistani yaongezeka

14 Novemba 2014

Mapigano kati ya India na Pakistan kuhusiana na eneo la Kashmir yameongezeka na kufikia kuwa janga la kibinaadamu.

https://p.dw.com/p/1Dbt7
Pakistan Demonstration von Imran Khan Anhängern in Gujranwala
Picha: picture-alliance/dpa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu vifo pamoja na ongezeko la idadi ya watu kupoteza makazi yao wakati mashirika ya haki za binaadamu yakionya kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu za kimataifa endapo madai kwamba mapigino hayo yanawalenga raia ni ya kweli.

Ulikuwa usiku mtulivu, pale ambapo kombora liliposhambulia eneo la makazi ya Shahdin Mohammad, na kusababisha vifo vya mtoto wake na mjukuu wake na kuwajeruhi wengine watatu katika familia hiyo. Mkasa huo ulitokea wakati baadhi ya wanafamilia wakiwa wamelala nje nyumba yao.

Mohammed akiwa kapiga magoti huku akimwonesha mjukuu wake wa miaka 12, alipiga mayowe ya kutaka msaada, lakini wakati majirani walipofika katika eneo hilo na kuwapeleka katika hospitali iliyo karibu, walikuwa washachelewa.

Mohammed mwenye umri wa miaka 65, mkulima wa Kihindi kutoka katika shamba la kijiji liitwacho Jeora alisema, na hapa namnukuu" Mashambuli yalianza saa nane usiku na hatukuwa na mahala pakwenda. Tulikuwa nyumbani kwetu wakati kombora lilipotua mbele yetu. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Dunia kwangu mimi" Alisema bwana huyo.

Umbali wa kiasi cha kilometa moja kutoka mpaka mwa India na Pakistani ndipo lilipo shamba la Jeora ambalo ni alama ya vijiji vyenye mgogoro ndani ya eneo la Kashimir ambalo limekuwa likipiganiwa na kuongeza mapigano kati ya nchi hizo mbili.

Kaschmir Studenten von Universität entlassen
waandamanaji kutoka eneo la KashmirPicha: Arif Ali/AFP/Getty Images

Wakati wa miaka 11 ya mapumziko ya mapigano pamoja na kunyoosha mipaka baada ya mwaka 2003 kusitisha mapigano, vijiji vilikuwa pande zote na kujenga majengo ya matofali yaliyochukua nafasi ya vibanda vya matope, shule na kumbi za harusi zilifunguliwa karibu na vituo vya ukaguzi lakini amani hiyo sasa imesambaratika.

Mwezi wa nane ni wakati ambao familia ya Mohamed iliuwawa. Mapigano yaliendelea kwa siku 45 na kuathiri uzalishaji wa mchele, na masomo kwa watoto wengi na mwezi huu mapigano yameanza upya.

Kombora lilirushwa kama kawaida baada ya vikwazo vya jeshi na kuua raia 23 mwaka huu, na kufanya idadi kubwa ya vifo ndani ya muongo mmoja na kusababisha mashitaka ya makusudi yaliyowalenga raia.

Katika mapigano ya hivi karibuni ya nchi hizo jirani zinazomiliki silaha za nyukilia Wapakistani tisa na wahindi wanane waliuwawa

India na Pakisttan zimepigana vita mara tatu tangu zipate uhuru kutoka kwa Uingereza 1947, mara mbili kupigania eneo lenye idadi kubwa ya waislamu la Kashmir na milima yake ya Himalaya na mabonde yenye rutuba ambayo nchi hizo zinadai kuwa himaya zao, lakini zinatawala kwa sehemu.

Indien Zubin Mehta mit dem Orchester der Bayerischen Staatsoper in Srinagar 07.09.2013
polisi nchini India wakiwadhibiti wandaamanajiPicha: ROUF BHAT/AFP/Getty Images

Ingawa mashambulizi ya risasi ya kulipiza kisasi yamelikumba eneo la udhibiti lisilo na shughuli za kijeshi, ambalo linalitenganisha eneo la Kashmir linalomilikiwa na India na eneo la Kashmir linalomikiwa na Pakistan, mapigano yamezidi kuchacha.

Maafisa wa Jeshi la India wamesema mpaka sasa Pakistan imekiuka makubaliano zaidi ya 110 ya kusitisha mapigano mwaka huu ikilinganishwa na 347 mwaka 2013 na 114 mwaka 2012.

Serikali ya Pakistan imesema India imekiuka makubaliano 227 ya kuweka chini silaha kwa mwaka huu, na makubaliano 414 mwaka uliopita na mengine 230 kwa mwaka 2012. Lakini Waziri Kiongozi wa India anayetawala eneo la Kashmir ameituhumu Pakistan kwa kubadili mbinu za kivita na kuwalenga raia.

Katika eneo la Tambarare lenye kufanyika kilimo cha mpunga, wenye kutoa aina maarufu ya mchele aina ya Basmati, mapigano ya muda yamewalazimu maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kuishi katika shule ambazo zimegeuzwa kuwa kambi za kutolea misaada, jambo ambalo limeyavuruga maisha ya kila mmoja kuanzia watoto hadi wakulima.

Watoto wanalalamika kutoweza kwenda shule na kusema wanahofia sana kutoka nje kutokana na silaha zinazovurumishwa kimya kimya katika maeneo yao.

Mwandishi: Nyamiti Kayora/RTRE

Mhariri: Josephat Charo