1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano kati ya majeshi ya DRC na Rwanda

12 Juni 2014

Mapigano makali yameripotiwa kati ya mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda hii leo. Mapigano hayo yalioanza jana kati ya wanajeshi wa nchi hizo mbili yamesemekana kusababisha mauaji ya wanajeshi kadhaa.

https://p.dw.com/p/1CH9a
Wanajeshi wa DRC
Wanajeshi wa DRCPicha: DW/John Kanyunyu

Pande zote mbili zinalaumiana kwa kuanzisha mapigano hayo. Kwa sasa wakaazi wa maeneo hayo wanahofia usalama wao wakiomba viongozi wa nchi hizo kusawazisha hali ya mambo ili utulivu urejee katika nchi hizo za Afrika ya kati. Sylvanus Karemera ni mwandishi wetu ambaye kwa sasa yuko kwenye eneo la mpakani na kwanza anaelezea hali ilivyo kwa sasa.. Kusikiliza ripoti yake bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sylvanus Karemera

Mhariri:Yusuf Saumu