1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano Kivu ya kaskazini

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GL

Kinshasa:

Mashirika ya misaada ya kiutu yanasema yameingiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na maelefu ya raia waliotawanyika wakikimbia mapigano ya Kivu ya kaskazini.”Kuna shida ya kuwafikia watu hao kutokana na mapigano hayo”-taarifa ya ofisi inayosimamia shughuli za mashirika ya misaada ya kiutu katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-Ocha, imesema.Mapigano yameripuka upya tangu Agosti iliyopita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaoongozwa na Laurent Hunda.Watu zaidi ya laki tatu na nusu wameyapa kisogo maskani yao-taarifa hiyo inasema.Wakati huo huo mapigano yanaripotiwa kuendelea pia hii leo katika miji ya kaskazini mwa Goma,mji mkuu wa Kivu ya kaskazini.Mapigano haya yanaendelea licha ya mwito wa kiongozi wa waasi Laurent Hunda wa kuweka chini silaha.Na Rwanda imekanusha hii leo ripoti zinazodai wanajeshi wake wanakutikana katika eneo hilo la mapigano.