1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mapya yazuka tena mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cyqc

KINSHASA:

Mapigano mapya yameripoti mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,licha ya mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa sahihi wiki iliopita.

Mapigano hayo yanasemekana kuwa kati ya waasi wa Kitutsi wa Congo dhidi ya wapiganaji wa MaiMai.

Mapigano inasemekana kutokea leo karibu na vijiji vilivyoko umbali wa kilomita 70 magharibi mwa mji wa Goma.Wapiganaji wa Kitutsi watiifu kwa Gerali Muasi Laurent Nkunda na wanamgambo wa Mai mai wa Pareco wamepiagana leo na kila upande unaulaumu mwingine kwa kuanzisha mapigano hayo.makundi yote mawili yalitia sahini mkataba wa amani ambapo makundi husika yalikubaliana kusitisha mapigano mara moja.Msemaji wa kijeshi wa kundi la laurent Nkunda,Seraphin Mirindi ameliambia shirika la habari la AFP kuwa huu ni ukiukwaji wa mkataba wa amani. Nae msemaji wa Pareco Maimai-Theopihile Museveni akwa upande wake akawalaumu waiganaji wa Nkunda.Jeshi la Umoja wa matifa linalolinda amani nchini Kongo la MONUC halijui nani alieanza mapigano ya sasa.