1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mjini Basra Iraq yapamba moto

Kalyango Siraj26 Machi 2008

60 wafariki na wengine 200 wajeruhiwa kufikia sasa

https://p.dw.com/p/DUpi
Kiongozi wa kidini wa Kishia Muqtada al-Sadr akiwahutubia wafuasi wake mjini Basra, kilomita 550 kusini mashariki mwa Baghdad, Iraq, mwaka wa 2006.Wapiganaji wake wa jeshi la Mahdi wanapambana dhidi ya majeshi ya serikali na ya Marekani katika miji ya Baghdad na BasraPicha: AP

Waziri mkuu wa Iraq amewapa siku tatu wale wote waliona silaha kinyume na sheria kati mji wa Basra wawe wamezisalimisha silaha hizo la sivyo watachukuliwa hatua kali.

Onyo hilo limekuja wakati kukiwa nataarifa za kuendelea kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kundi la Mahdi ambapo inaarifikiwa watu kadhaa wameuawa huku takriban 50 kujeruhiwa.

Wapiganaji watiifu kwa kiongozi wa kidini wa Kishia,Moqtada al-Sadr wameigana na majeshi ya serikali ya Iraq pamoja na ya Marekani kwa siku ya pili leo jumatano katika miji ya Baghdad na Basra wakati zoezi la kuyapokonya silaha makundi haramu hashasa dhidi ya kundi la mgambo lenye nguvu kuliko yote nchini humo.

Idadi ya wahanga wa mapigano haya sasa inasemekana kufikia vifo vya watu 60 na waliojeruhiwa wamefika 200.

Mapigano ya kwanza kati ya wapiganaji wa kundi la Mahdi yalianza usiku wa manane katika kiunga cha mji wa Baghdad cha Sadr City ambako wanapatikana kwa wingi wapiganaji hao.Afisa mmoja katika hospitali ya karibu na hapo inayoitwa Imam Ali amesema kuwa watu wanne wameuawa na 24 kujeruhiwa katika kiunga cha mji huo kilichoko kaskazini magharibi na kinakadiriwa kuwa na watu wapatao millioni mbili.

Walioshuhudia wanasema mapigano kati ya wanamgambo hao na wanajeshi wa Iraq pamoja na ya Wamarekani ya hapa na pale yameendelea.

Pia mapigano yalitokea milango ya alfajiri ya leo jumatano mjini Basra kati ya wapiganaji hao dhidi ya vikosi vya Iraq,hatua iliomulazimisha waziri mkuu Nuri al -Maliki kutoa onyo kwa wapiganaji hao.

Mshauri wake Sadiq al-Rikabi amesema kuwa waziri mkuu ametoa mda wa saa 72 ambazo ni sawa na siku tatu wasalimishe silaha zao na pia kutia sahihi mkataba wa kuachana na vitendo vya ghasia.

Mshauri huyo amesema kuwa mtu yeyote mwenye silaha atakaeshindwa kusalimisha silaha yake kwa kituo cha polisi ifikapo Ijumaa atachukuliwa hatua muafaka kama vile kukamatwa.

Mapigano yalianza jana alhamisi katika mji wa kusini wenye utajiri wa mafuta wa Basra ,baada ya serikali ya Baghdad kuamuru kuyashughulikia magenge yenye silaha katika mji huo.

Polisi inasema kufikia sasa wanamgambo 218 ndio wamekamatwa tangu operesheni hiyo ianze.

Kiongozi wa kidini jana alionya kuchukua hatua ikiwa hujuma dhidi ya watu wake itaendelea.Moqtada alisema kuwa operesheni hiyo inalenga vijana wake.Lakini msemaji wa serikali Ali al-Dabbagh amekanusha hayo.

Msemaji wa jeshi la Marekani amesema kuwa mizinga kadhaa ilivurumishwa katika eneo linalolindwa mjini Baghdad la Green Zone na wale aliowaita magaidi.Amesema kuwa mizinga hiyo imefyatuliwa kutoka mtaa wa Sadr City wenye washia wengi.

Nao maafisa wa Iraq wamesema jumatano kuwa mizinga zaidi imevurumishwa katika Green Zone.Wameongeza kuwa mzinga mmoja umelipiga jengo moja nje ya eneo hilo ambapo limemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wanne.

Habari za hivi punde zinasema kuwa raia watatu wa Marekani wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mizinga.

Mapigano ya sasa yanatilia wasiwasi na kushuku amri ya kusitisha mapigano alioitoa Moqtada al-Sadr mwezi Agosti na kurejelewa mwezi uliopita.