1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaendelea Libya

Halima Nyanza(ZPR)18 Agosti 2011

Majeshi ya serikali ya Libya na yale ya waasi wa nchi hiyo, bado yanaendelea na mapigano, ikiwa ni miezi sita sasa tangu kuzuka kwa upinzani, dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/12IbS
Wapiganaji waasi katika mji wa ZawiyahPicha: dapd

Majeshi ya Gaddafi yamekuwa yakipambana na waasi katika kuudhibiti mji wa Zawiyah, ulioko magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

Mapigano makali yameripotiwa kutokea karibu na mji huo wa Libya ambao unakiwanda cha kusafisha mafuta yanayosambazwa katika mji mkuu wa Tripoli pamoja na gesi.

Libyen Al-Sawija
Baadhi ya majengo yaliyoharibiwaPicha: picture alliance/dpa

Mji huo wa Zawiyah ni muhimu pia kwa serikali ya Libya kutokana na kuwa katika njia kuu iliyokiungo muhimu kwa Tripoli, katika usambazaji wa vitu mbalimbali nchini humo.