1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka tena.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW3r

Kivu, jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , waasi wamedai kuwa wameyashambulia majeshi ya serikali na kuyaondoa katika vijiji viwili. Duru za umoja wa mataifa zinasema kuwa mapigano baina ya jeshi la Kongo na waasi wanaoongozwa na jenerali wa zamani Laurent Nkunda yalianza mapema jana Jumapili katika kijiji cha Kikuku katika jimbo la Kivu ya kaskazini. Mapigano hayo baadaye yalisambaa katika mji wa Nyanzale, ambako kikosi cha jeshi la serikali kilikuwapo. Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa wengi wa wakaazi wapatao 40,000 wa Nyanzale pamoja na maeneo yanayozunguka eneo hilo wamekimbia mapigano hayo. Mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wanashutumu pande zote mbili kwa kuhusika na makosa dhidi ya ubinadamu dhidi ya raia.