1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO:Baba mmoja avuliwa haki za ulezi

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjS

Mtoto mmoja wa kike aliyepata umaarufu kwa kuzaliwa juu ya mti wakati nchi ya Msumbiji ilipokumbwa na mafuriko mwaka 2000 ameshinda kesi inayomnyima babake haki za ulezi.Kwa mujibu wa redio ya kitaifa ya Msumbiji mahakama iliamua kuwa babake mtotto huyo Rosita Mabuiango aliiba na kuzuiza bidhaa alizopewa kama msaada kwa familia yao.

Rosita aliye na umri wa miaka 7 sasa alizaliwa juu ya mti mwezi Februari mwaka 2000 baada ya Mto Limpopo uliojaa mamba kufurika.Watu 700 walipoteza maisha yao katika mafuriko hayo.

Kisa hicho kilitangazwa kwenye televisheni moja ya kimataifa jambo lililochangia pakubwa kuhamasisha jamii ya kimataifa kutoa msaada wa takriban dola milioni 500 kwa wahanga wa mkasa huo.

Kituo cha Redio cha Msumbiji kinatangaza kuwa msaada iliyopewa familia hiyo vikiwemo friji,mifugo, jenereta na kifaa cha kunasa nishati ya jua..yaani solar panel viliibiwa na babake mtotto huyo Salvador Mabuiango na kuuzwa.Mahakama hiyo inamruhusu mamake Rosita Bi Sofia Mabuiango kuwa mmiliki pekee wa mali ya msichana huyo mdogo.