1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO:Kimbunga Favio chagonga katikati ya Msumbiji

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPi

Kimbunga Favio kilicho na pepo za kasi ya kilomita 200 kwa saa kimepiga eneo la kati la Msumbiji na kusababisha mvua kali na matatizo mapya kwa maelfu ya wakazi wa eneo hilo walioathiriwa na mafuriko tangu wiki jana.Kimbunga cha pili Gamede kiko baharini kaskazini mashariki mwa kisiwa cha Madagascar na kutishia kupiga eneo la katikati la Msumbiji kabla kesho.

Kimbunga hicho kimeharibu nyumba na kupeperusha mapaa katika eneo la Vilankulo kusini mwa Beira.Serikali imewaondoa wakazi wengi katika eneo hilo na kuwapeleka katika maeneo yaliyo juu zaidi .Wakazi waliosalia walitia juhudi kuokoa mali zao katika nyumba zao zilizoharibiwa na kimbunga hicho.