1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO.Msaada wa chakula waanza kutolewa

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSZ

Shirika la chakula la umoja wa mataifa WFP limeanza kugawa msaada wa dharura wa chakula kwa maelfu ya wahanga wa mafuriko ya Msumbiji.

Takriban watu elfu sabini wamehamishwa kutoka kwenye makaazi yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Maeneo ya Zimbabwe, Zambia na Malawi pia yanakabiliwa na mvuy hizo kubwa.

Sehemu zilizo karibu na mto Zambezi zimeathiriwa zaidi na mafuriko.