1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais wa Kongo na Rwanda wajadili suali la mashariki ya Kongo

26 Septemba 2012

Pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na marais Joseph Kabila wa Kongo na Paul Kagame wa Rwanda walikaa kujadiliana juu ya hali mashariki ya Kongo.

https://p.dw.com/p/16Egk
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rais Paul Kagame wa RwandaPicha: picture-alliance/dpa

Clinton aliwasisitizia viongozi hao wawili kuutatua mgogoro kuhusiana na suala la waasi katika eneo hilo.Aidha leo marais hao wanatazamiwa kukutana na viongozi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika mkutano maalum juu ya mzozo katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.Rais Kabila aliyetoa hotuba yake hapo jana mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ameutaka Umoja huo utimize wajibu wake katika kuwashinikiza watu na nchi zinazohusika na machafuko ya Kivu.Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo yuko New York na ametutumia taarifa ifuatayo.

(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi