1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuondoa majeshi yake kutoka Irak mwaka ujao

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cf5s

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amesema Marekani itaondoa vikosi vyake vitano vya wanajeshi karibu 20,000 kutoka nchini Irak ifikapo katikati ya mwaka ujao 2008.

Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka na waandishi wa habari, waziri Robert Gates amesema hilo litawezeka kwa sababu ya ufanisi uliofikiwa na wanajeshi katika kudumisha usalama.

Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema machafuko nchini Irak yamepungua kufuatia hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi kufikia 160,000.

Wakati huo huo, rais wa Poland, Lech Kacynski, ameidhinisha kuondoka kwa wanajeshi wa Poland kutoka Irak ifikapo mwezi Oktoba mwaka ujao.

Waziri mkuu mpya wa Poland, Donald Tusk aliahidi wakati wa kampeni yake kuwaondoa wanajeshi wa Poland kutoka Irak wakati atakapoingia madarakani. Poland ina wanajeshi 900 nchini Irak.