1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kutumia dola bilioni 819 kuupiga jeki uchumi

Thelma Mwadzaya29 Januari 2009

Baraza la wawakilishi la Marekani lililo na wanasiasa wengi wa chama cha Democratik limeidhinisha mpango wa kuupiga jeki uchumi utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 819.

https://p.dw.com/p/GiGg
Ikulu ya Whitehouse ya MarekaniPicha: AP

Uamuzi huo umeungwa mkono kwa kura 244 za upande wa Demokratik na kupingwa na upande wa Republikan kwa kura 188.Rais Barack Obama wa Marekani alisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua hiyo ili kuyanusuru maisha ya raia wa kawaida


Mswada huo ulipingwa na wanachama 11 pekee wa Demokratik na kuungwa mkono na waliosalia.Upande wote wa Republikan uliupinga mswada huo.Mswada huo unasubiri kujadiliwa na Baraza la Senate wiki ijayo.