1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na juhudi za kumkomboa raia wake kutoka kwa Maharamia.

Halima Nyanza/DPA/Reuters10 Aprili 2009

Manowari zaidi za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani zinaelekea katika pwani ya Somalia ili kuwashinikiza zaidi Maharamia kumuachia Nahodha wa Meli, iliyokamatwa kwa muda na maharamia hao mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/HUJe
Baadhi ya Maharamia wa Kisomali waliokamatwa, kwa sasa wanadaiwa kushuka katika pwani ya Mashariki mwa Afrika.Picha: AP

Wakati hayo yakiendelea, taarifa zikisema kuwa Meli ya Maersk Alabama inaelekea Kenya kwa sasa, chini ya Ulinzi wa Jeshi la Marekani, baada ya mabaharia kuwazidi nguvu maharamia hao.


Wakati ambapo Jeshi la Wanamaji la Marekani linajiimarisha zaidi kuwashinikiza Maharamia hao, kuweza kumuachia Nahodha huyo wa Meli, Richard Philips ambaye bado anashikiliwa mateka ndani ya mashua ya uokoaji ya meli hiyo, ikiwa ni siku ya pili sasa tangu alipokamatwa, Majadiliano kati ya Maharamia na Jeshi hilo la Wanamaji bado yanaendelea.


Maafisa wa jeshi la Marekani, wamesema manowari za kivita zaidi zinapelekwa kuongeza nguvu ili kusaidia kuachiwa kwa usalama kwa mateka huyo.


Jeshi la Marekani limetuma vikosi zaidi katika eneo hilo, ambalo Maharamia wa Kisomali siku ya Jumatano waliiteka teka meli hiyo, lakini hata hivyo wafanyakazi wapatao 20 wa meli hiyo ya Maersk Alabama, ambao pia ni raia wa Marekani, walifanikiwa tena kuidhibiti.


Habari zinasema meli hiyo iliyolengwa kukamatwa na maharamia hao, iliondoka jana katika eneo iliyopo mashua hiyo ya uokoaji anamo shikiliwa nahodha huyo, ikiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Wanamaji wa Marekani, huku wafanyakazi wake wote wakiwa salama, ukiondoa nahodha wale ambaye bado anashikiliwa.


Akizungumza na DW, leo Andrew Mwangura mratibu wa Shughuli za Mipango ya Safari za Meli katika pwani ya Afrika Mashariki amesema meli hiyo inatarajiwa kufika kesho katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.


Katika hatua nyingine, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Roberts Gates, amewaambia waandishi wa habari mjini Washngton, kwamba kipaumbele kikubwa kwao ni kurudishwa salama kwa nahodha huyo.


Meli hiyo ilikumbwa na mkasa huo siku ya Jumatano, kiasi cha kilomita 500 kutoka katika pwani ya Somalia wakati ikielekea katika bandari ya Mombasa nchini Kenya, ikiwa imebeba msaada wa chakula kwa ajili ya wakimbizi.