1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yafuraia kushindwa kwa jaribio la Chavez kubadili katiba

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWTh

WASHINGTON.Marekani umeupongeza uamuzi wa wananchi wa Venezuela kuyakataa mapendekezo ya Rais Hugo Chavez ya marekebisho ya katiba, katika kura iiliyofanyika Jumapili iliyopita.

Imesema kuwa matokeo ya kura hiyo ni mustakhbali mzuri kwa uhuru na demokrasia ya nchi hiyo.

Rais Chavez alitangaza kuyakubali matokeo hayo akishindwa kwa asilimia moja, hatua ambayo iliwashangaza si tu wafuasi wake bali hata wapinzani wake.

Kiongozi huyo aliwapongeza wapinzani wake kwa kushinda , lakini akasisitiza kuwa ataendelea na mapambano ya kuujenga usoshalisti na kwamba mapendekezo yake hayo bado yako hai.

Chavez amutoa wito kwa wafuasi wake kuwa watulivu, baada ya kushindwa kwa jaribio la kutaka kubadilisha katiba ambayo yangetoa nafasi ya kutokuwepo kwa ukomo wa kuwania urais