1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yailaumu Iran kwa tukio la uchokozi.

8 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CmRb

Washington.Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema kuwa Iran imefanya kitendo cha hatari wakati maboti yaendayo kasi matano ya nchi hiyo yalipozingira meli tatu za kijeshi za Marekani na kutishia kuzilipua katika eneo la mlango bahari la Hormuz jana Jumatatu.

Wairan hao walidondosha maboksi katika sehemu iliyokuwapo meli lakini waliondoka kabla ya kamanda wa meli moja ya kijeshi kutoa amri ya kushambulia. Serikali ya Iran imekanusha tukio hilo, ikisema ni kitu cha kawaida. Gates amesema kuwa mpango bahari huo ni eneo tete na nafasi ya tukio la kijeshi inaonengezeka. Kiasi cha robo ya mafuta ghafi duniani yanasafirishwa kupitia mlango bahari huo.