1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya tena Sudan kuhusu Darfur

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbiJ

Marekani imetishia kuiwekea Sudan vikwazo vipya vya Umoja Mataifa. Na baada ya kikao cha usalama cha Umoja wa Mataifa mjini New York, balozi wa Marekani, Zalmay Khalilzad, ameilaumu serikali ya Sudan kwa kusababisha kuchelewa kupelekwa kwa vikosi vya mseto wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur. Askari wa vikosi hivyo wanafikia elf 26.Balozi amesema kuwa ikiwa utawala wa Khartoum hautakubali kujumulishwa kwa askari kutoka Thailand, Nepal na Scandinavia katika kikosi hicho ili kukiimarisha,baraza la usalama litaichukuilia hatua ya kuiwekea vikwazo.Kazi kuu ya Umoja wa Mtaifa huko Darfur, ni kujaribu kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameendelea kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.Watu wanaokadiriwa laki mbili wameuliwa na wengine zaidi ya millioni 2 kuachwa bila makazi.