1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaishambulia IS Syria

Admin.WagnerD23 Septemba 2014

Marekani imepanua operesheni yake dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria, ikisaidiwa na mataifamatano ya Kiarabu - Bahrain, Qatar, Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu.

https://p.dw.com/p/1DHOk
Symbolbild Algerien Geiselnahme Islamischer Staat Franzose
Picha: picture-alliance/AP

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London limesema mashambulizi hayo yalilenga mkoa wa kaskazini wa Raqq na pia mji mkuu wake. Ukanda wa video uliyowekwa mtandaoni leo, unaonesha mabomu yakidondoka katika eneo la wazi, miripuko inayosemekana kutokana na mashambulizi ya washirika. Msimulizi katika ukanda huo anasikika akisema unaonyesha mashambulizi kwenye kijiji cha Kfar Derian, huku akitamka Allah Akbar, yaani Mungu mkubwa.

Syrien IS Kämpfer in Raqqa
Wapiganajiwa IS nchini Syria.Picha: picture-alliance/AP Photo

Wanaharakati wamesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo ndani na nje ya mji wa Raqqa nchini Syria, na kuongeza kuwa yalisababisha maafa miongoni mwa wapiganaji wa Dola la Kiislamu. Mji wa Raqqa ndiyo uliyotangazwa na kundi hilo la wapiganaji kuwa mji mkuu wao nchini Syria. Mwanaharakati mwigine alieko mkoa wa kaskazini wa Idlib, alithibitisha kuwa makombora kadhaa yaliushambulia mji wa Kfar Derian katika saa za asubuhi leo Jumanne. Mashambulizi yore yaliwalenga wapiganaji wa IS pamoja na wale kundi lenye mafungamano na mtandao wa Al-Qaeda la Al-Nusra Front.

Syria yasema iliarifiwa

Ndege za Marekani pia zilifanya mashambulizi 30 katika mkoa wa Deir al-Zour mashariki mwa Syria, unaopakana na Iraq. Serikali ya Syria ilisema iliafiriwa mapema juu ya mashambulizi ya Marekani. Shirika la habari la Syria, likiinuku wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, limesmea kuwa upande wa Marekani ulimuarifu balozi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba kungefanyika mashambulizi dhidi ya Dola ya Kiislamu mkoani Al-Raqqa.

Uamuzi wa kufanya mashambulizi ulichukuliwa mapema siku ya Jumatatu na kamandi kuu ya Marekani kwa idhini ya rais Baracl Obama. Mashambulizi hayo ndiyo yalikuwa ya kwanza dhidi ya Dola ya Kiislamu nchini Syria. Marekani ilishafanya mashambulizi dhidi ya kundi hilo nchini Iraq, lakini ilisema ingelifuata ndani ya Syria ikibidi.

Maafisa wa Marekani walisema mashambulizi hayo yalianza saa tisa Alfajiri, na yalifanywa na Marekani, Bahrain, Qatar, Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu. Mkuu wa upinzani unaoungw amkono na mataifa ya magharibi Hadi Bahra, alikaribisha kuanza kwa mashambulizi nchini Syria. Viongozi wa kijeshi wamesema theluthi mbili ya wapiaganaji wanaokadiriwa kufikia 31,000 wako nchini Syria, lakini baadhi ya maafisa wameelezea wasiwasi kuwa mashambulizi hayo yanaweza kumsaidia rais Assad ,kwa sababu hao wanapigana kwa sehemu kumn'goa yeye.

Marekani imepanua operesheni yake dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria, ikisaidiwa na mataifamatano ya Kiarabu - Bahrain, Qatar, Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Wapiganaji wa IS wakiwa mjini Raqqa.Picha: picture-alliance/AP Photo

Ufaransa yasema itamkomboa raia wake

Wakati huo huo, Ufaransa imesema kuchukuliwa mateka kwa raia wake nchini Afghanistan hakutaizuwia nchi hiyo kushiriki operesheni za muungano wa mataifa zinazoongozwa na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislamu, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius amewambia waandishi wa habari.

"Nia ya Ufaransa inaendelea kuwa ile ile: Tuna mpango wa kufanya kadiri tuwezavyo kuwaokoa mateka, na hasa mateka huyo lakini kundi moja la kigaidi haliwezi kushawishi msimamo wa Ufaransa," alisema waziri Fabius.

Raia huyo wa Ufaransa alitekwa mashariki mwa Algeria siku ya Jumapili, na watekaji wake walitoa mkanda wa video wakitishia kumuuwa ikiwa Ufaransa haitasitisha uingiliaji wake kijeshi nchini Iraq inakounga mkono operesheni ya Marekani dhidi ya IS.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre,dpae,ape

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman