1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapeleka manowari ya kivita pwani ya Libanon

29 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DFf6

WASHINGTON:

Markeani imetuma manowari yake ya kijeshi "USS Cole" kupiga doria katika pwani ya Lebanon.Kwa mujibu wa afisa mmoja wa kijeshi,manowari hiyo itasaidia kuleta utulivu katika kanda hiyo.Lakini serikali mjini Washington ilikataa kutamka iwapo manowari hiyo inapelekwa kama onyo kwa Syria,nchi inayotuhumiwa na Marekani kuwa inaingilia mambo ya ndani ya Lebanon.

Mgogoro wa kisiasa kati ya serikali ya Lebanon inayoelemea kambi ya Magharibi na chama cha Hezbollah kinachoiunga mkono Syria,umekwamisha majadiliano kati ya pande hizo mbili na nchi hiyo haina rais tangu mwezi Novemba mwaka jana.