1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashindwa kutuliza mashaka ya Ulaya kwa Trump

20 Februari 2017

Mwezi moja baada ya kuchaguliwa kwa Trump mawaziri wake waandamizi wamepelekwa Brussels makao makuu ya Umoja wa Ulaya,Bonn na Munich nchini Ujerumani wiki hii kuihakikishia Ulaya kwamba kila kitu kitakuwa sawa.

https://p.dw.com/p/2Xvsb
Deutschland | Münchner Sicherheitskonferenz | Außenminister aus der Ukraine Pavlo Klimkin, Frankreich  Jean-Marc Ayrault, Russland Sergey Lavrov und Deutschland Sigmar Gabriel
Picha: REUTERS/S. Hopp

Mataifa hayo ya Ulaya yameelezwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis kwamba muungano wa kijeshi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO sio "umepitwa na wakati " licha ya Trump kudokeza hivyo mara kadhaa.

Na wakaja kuambiwa na Makamo wa Rais wa Marekani Mike Pence kwamba Russia "itawajibishwa" kwa vitendo vyake nchini Ukraine licha ya ishara za kujipendekeza Trump kwa Rais Vladimir Putin wa Russia.

Lakini iwapo ziara za mawaziri hao ilikuwa ni kuihakikishia Ulaya kwamba nguzo za sera ya kigeni ya Marekani haikuyumba iko vile vile kama ilivyo wameshindwa kuthibitisha hayo huo ndio mtizamo wa wanadiplomasia wa Ulaya,wanasiasa na wachambuzi waliokutana mjini Munich kwa ajili ya mkutano wa usalama.

Ruprecht Polenz mkuu wa zamani wa kamati ya masuala ya kigeni katika bunge la Ujerumani ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters baada ya hotuba ya Pence katika mkutano wa usalama wa Munich kwamba "Kile tulichokisia hapa hakitowi hakikisho. Hakuna kabisa dira yenye kuonyesha vipi tutashirikiana na kupiga hatua."

Amwakilisha Trump

Münchner Sicherheitskonferenz 2017 | Mike Pence, USA
Makamo wa rais wa Marekani Mike Pence akihutubia katika mkutano wa Munich.Picha: Reuters/Bundesregierung/G. Bergmann

Pence alikuwa afisa mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa wa serikali ya Trump kusafiiri kuja Ulaya na hotuba yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu.Miaka minane iliopita katika ukumbi huo huo wa Munich mtangulizi wake Joe Biden aligonga vichwa vya habari kwa kuahidi kurekebisha upya uhusiano na Russia.

Makamo wa rais wa hivi sasa alijaribu kukabiliana na mashaka hayo ana kwa ana kwa kuweka wazi mwanzoni wa hotuba yake kwamba alikuwa akizungumza kwa niaba ya Trump.

Lakini baadae alimtaja rais huyo mara 19  katika hotuba yake ya dakika 20 na kumfanya mmojawapo wa wasikilizaji mwandishi na mtaalamu wa historia Robert Kegan kuipuuza hotuba hiyo kuwa ya "saluti ya roboti kwa kiongozi aliyeko madarakani."

"Pence na Mattis na Tillerson wanaweza kuja hapa na na kuzungumzia umuhimu wa uhusiano wa Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na hilo ni jambo zuri" amesema hayo Elmar Brok mkuu wa kamati ya masuala ya kigeni ya bunge la Ulaya na mshirika wa chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.

Amesema hawajuwi nini kinachokuja kwenye mtandao wa Twitter hapo kesho akimaanisha tabia ya Trump kumwaga sera za uatawala wake kupitia mtandao wa kijamii.

Mwandishi : Mohamed Dahman/Reuters

Mhariri  : Mohammed Abdul-Rahman