1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatatiza juhudi za mchakato wa uongozi wa WTO

Tatu Karema
29 Oktoba 2020

Mchakato wa Shirika la Biashara Duniani WTO wa kuchagua kiongozi mpya umekwama baada ya Marekani kumkataa mwanamke wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala aliyependekezwa kama mkurugenzi mkuu wa shirika hilo.

https://p.dw.com/p/3kbfi
Ehemalige Außen- und Finanzminister Ngozi Okonjo-Iweala
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Utawala wa Rais Donald Trump tayari umeshadhoofisha uwezo wa shirika hilo la WTO kama msuluhishi wa masuala ya kibiashara ulimwenguni kwa kuzuia teuzi za jopo lake la rufaa. Na sasa linatishia kukwamisha uteuzi wa uongozi wa shirika hilo kwa wiki au miezi kadhaa ijayo. Shirika hilo la WTO limeitisha mkutano mnamo Novemba 9, ambapo linatarajia litakuwa limeshapata uungwaji mkono wa kutosha wa kuteuliwa mgombea huyo kutoka Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala.