1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa watano wahamishwa kutoka Guantanamo

Ambia Hirsi16 Novemba 2015

Watu watano ambao wamekuwa wakizuiliwa na Marekani katika gereza la Guantanamo nchini Cuba kwa zaidi miaka 13 hatimaye wamehamishwa na kupelekwa katika Umoja wa Falme ya nchi za Kiarabu. Ambia Hirsi na maelezo zaidi

https://p.dw.com/p/1H6Tq
Guantanamo Camp 4 Symbolbild CIA Folterprogramm
Gereza la GuantanamoPicha: picture-alliance/ZUMA Press

Watu watano ambao wamekuwa wakizuiliwa na Marekani katika gereza la Guantanamo nchini Cuba kwa zaidi miaka 13 hatimaye wamehamishwa na kupelekwa katika Umoja wa Falme ya nchi za Kiarabu . Hayo yameripotiwa na Wizara ya ulinzi ya marekani.

Wafungwa hao, waliyotambuliwa kama Ali Ahmad Muhammad al-Razihi, Khalid Abd-al-Jabbar Muhammad Uthman al-Qadasi, Adil Said al-Hajj Ubayd al-Busays, Suleiman Awad Bin Uqayl al-Nahdi, na Fahmi Salem Said al-Asani waliwasili katika UAE siku ya Jumamosi.Wafungwa hao watano raia wa Yemen wamepewa makazi mapya katika taifa la Ghuba ya Uajemi baada ya mamlaka ya Marekani kubainisha kuwa wao sio tishio tena,ilisema taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi ya marekani. Kuachiliwa kwa wafungwa hao kutoka gereza la Guantanamo kunafikisha 107 idadi ya wale waliyosalia kizuizini.

Hakuna hata mmoja kati ya wanaume hao watano ambaye amewahi kushtakiwa kwa uhalifu lakini walikuwa kizuizini kwa madai kwamba walikuwa wapiganaji hatari. Marekani inasema haikuweza kuwatumwa katika nchi yao kwa sababu Yemen ilikuwa na msimamo mkali kukubali wafungwa kutoka Guantanamo. Hawa ni wafungwa wa kwanza kukubaliwa na Falme za milki ya za kiarabu kwa makazi mapya.

Marekani yafuatilia wafungwa

Frankreich Terror in Paris Reax Obama
Rais wa Marekani Barak ObamaPicha: Reuters/K. Lamarque

Marekani anaendelea kuwafuatilia kwa jicho la karibu juuwale ambao wamekuwa wakitolewa, lakini baadhi ya takwimu inakadiria kuwa hadi asilimia 30 wafungwa hao hujiunga na makundi ya wapiganaji kwa lengo la kufanya mashambulizi dhidi ya nchi za Magharibi.

Gereza la Guantanamo hugharamu walipa ushuru wa marekani kati ya dola milioni 400-450 kwa mwaka, kulingana na makadirio.Ndiposa rais Barack Obama alifanya hoja ya kufunga Guantanamo ahadi muhimu ya uchaguzi, lakini akapingwa vikali na wabunge aliposhinda muhula wa pili wa uongozi wake. Obama amepunza idadi ya wafungwa katika gereza la Guantanamo kwa zaidi ya nusu tangu achukue hatamu wa ungozi wa taifa hilo lenye ushawishi mkubwa duniani.

Utawala wa Rais Obama hata hivyo unapania kuwapeleka wafungwa waliyosalia katika gereza la Guantanamo, nchini Marekani huku kukiwa na upinzani mkali juu ya suala hilo.Guantanamo bado inawazuia watuhumiwa watano wa mashambulizi ya Septemba 11, mwaka 2001 miongoni mwao ni mpangaji mkuu, Khalid Sheikh Mohammed.Gereza hili pia ni makaazi ya mshukiwa Abd al-Rahim al-Nashiri ambaye anatuhumiwa kuongoza mashambulizi ya USS Cole mnamo mwaka 2000. Abdal-Rahim al-Nashiri alikamatwa mwaka 2002 na kuhamishiwa Guantanamo 2006.

Mwandishi.Ambia Hirsi/APE/DPAE/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdulrahman