1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yazozana na Urusi juu ya waangalizi wa uchaguzi

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUxC

Ikiwa zimebakia siku chache tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Urusi Marekani imezozana na Urusi juu ya waangalizi wa uchaguzi.

Katika mkutano wa Jumuiya ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya OSCE mjini Madrid Uhispania waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema waangalizi wa uchaguzi wa jumuiya hiyo wanapendelea upande mmoja na kwamba Marekani imekuwa ikizuwiya kufanyika kwa mabadiliko kwenye chombo cha uangalizi wa uchaguzi wa jumuiya hiyo ya OSCE.Amesema mustakbali wa jumuiya hiyo ya Usalama na Ushirikiano barani Ulaya hauna matumaini makubwa iwapo tabia hazitobadilika.

Msaidizi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Nicolas Burns amesema mjumbe yoyote yule wa chombo hicho hapaswi kuwa na kitu chochote kile cha kuficha au kuwa na hofu.

Waangalizi wa uchaguzi wa jumuiya hiyo wamejitowa kufuatilia uchaguzi huo wa Urusi uliopangwa kufanyika Jumapili kwa kusema kwamba wamewekewa masharti mengi mno na serikali ya Urusi.