1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mark van Bommel kuwa kocha wa Wolfsburg

Josephat Charo
27 Mei 2021

Nahodha wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Mark van Bommel anatarajiwa kuwa kocha mkuu mpya wa Wolfsburg baada ya kocha Oliver Glasner kuhamia Eintracht Frankfurt.

https://p.dw.com/p/3u41T
Niederlande Fußball Feyenoord - PSV | Trainer Mark van Bommel
Picha: picture-alliance/Pro Shots/M. Keemink

Wolfsburg na raia huyo wa Uholanzi inaripotiwa wamekubaliana kwa sehemu kubwa juu ya kanuni na van Bommel atakayetambulishwa wiki iijayo baada ya kutia saini mkataba wake.

Mark van Bommel aliichezea Bayern kati ya 2006 na 2011. Timu nyingine alizowahi kuzichezea wakati wa kibaua chake cha kusakata kandanda ni PSV Eindhoven, Barcelona na AC Milan, huku akifanya kazi kama kocha na klabu ya PSV mpaka Desemba mwaka 2019.

Pia alitumia muda kama kocha msaidizi wa baba mkwe wake Bert van Marwijk katika timu za taifa za Saudi Arabia na Australia.

Glasner aliiongoza Wolfsburg katika mashindano ya kombe la mabingwa barani Ulaya, Champions, msimu uliopita, lakini uhamisho wake kwenda Frankfurt ulithibitishwa siku ya Jumatano.

(dpa)