1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutoka "nguruwe" hadi mgombea ukansela

Iddi Ssessanga
9 Juni 2017

Siasa ya Ujerumani na Martin Schulz - Hayo yanaweza kuunganishwa mpaka wakati huu katika neno moja: Würselen. Würselen ni mji mdogo wa karibu wakaazi 38,000 kaskazini mwa Aachen magharibi mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/2WObu
Deutschland Martin Schulz bei der SPD Bundestagfraktion
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Sohn

Huko ndiko alikokulia Martin Schulz mwenye umri wa miaka 62, na ndiko anakoishi mpaka sasa. Alikuwa meya wa mji huo kwa kipindi cha miaka 11 kuanzia 1987 hadi 1998, na alikuwa akiendesha duka la vitabu pamoja na dada yake.

'Nilikuwa nguruwe'

Wakati wa ujana wake, Martin Schulz pia alishuhudia nyakati ngumu mjini Würselen. Akizaliwa kwa baba ambaya alikuwa askari polisi Schulz ndiyo alikuwa mdogo zaidi miongoni mwa watoto watano. Alijiingiza katika ulevi akiwa kijana na hakuruhusiwa kuhitimu shule ya sekondari. Katikati mwa miaka ya 1970, akiwa na umri wa maiak 20, aliajiriwa kwa mwaka mmoja. Hii leo Schulz anazungumzia kwa uwazi historia yake. "Nilikuwa nguruwe, na sikuwa mwanafunzi mzuri," anasema.

Deutschland Martin Schulz bei der SPD Bundestagfraktion
MArtin Schulz na mwenyekiti wa SPD Sigmar Gabriel wakati wa kikao maalumu cha SPD mjini Berlin, 25.01.2017Picha: picture alliance/dpa/K. Nietfeld

Lakini pia alikuwa mashughuli katika chama cha SPD wakati huo. Alipochaguliwa kuwa meya wa Würselen katika umri wa miaka 32, hili lilimfanya kuwa kiongozi mdogo zaidi wa mji katika jimbo lote la North-Rhein Westphalia. Alichaguliwa mjumbe wa bodi ya utendaji ya SPD katika mji wa Aachen mnamo mwaka wa 1984 na ameiongoza bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 20 iliopita.

Schulz pia amekuwa mjumbe wa kamati ya taifa ya uongozi wa SPD tangu 1999, akihudumu kwenye bodi ya utendaji na kamati kuu  - na anasisitiza kwa majivuno kwamba kuwepo kwake katika kamati hiyo kwa miaka 18 kunamfanya kuwa mjumbe aliehudumu kwa muda mrefu zaidi.

Ni mwanasiasa wa kileo

Haiba yake ya wenyeji wa mto Rhein ambayo huoneka mara kwa mara humfanya mgeni mashuhuri katika mijadala ya televisheni.  Schulz hana kawaida ya kuogopa makabiliano, lakini yumkini hilo ndiyo humfanya mwanasaisa huyo mwenye umri wa miaka 62 kuonekana wa kileo inapokuja kwenye kujadili masuala ya kisiasa nyumbani Ujerumani.

Hivi karibuni aliliambia gazeti la Ujerumani la Süddeutsche kwamba haki na demokrasia vinahojiwa siku hizi, na kuogeza kuwa ukataji tamaa unatishia demokrasia, hasa pale watu wanapohisi kwamba demokrasia inaposhindwa kuwalinda watu wanatafuta njia mbadala.

Schulz pia huzungumza waziwazi inapokuja kwenye kupambana na kuenea kwa siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia, na mara kwa mara ameonyesha mjini Brussles na Strasbourg, kwamba anaweza kuyagusia masuala ambayo yanaweza kumkabili nyumbani Ujerumani.

Sonder-Fraktionssitzung der SPD Martin Schulz und Thomas Oppermann
Martin Schulz na kiongozi wa wabunge wa SPD Thomas Oppermann wakiwa katika kikao maalumu cha wabunge wa SPD katika bunge la Ujerumani Bundestag, mjini Berlin 25.01.2017.Picha: picture alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Kuhusu Urusi chini ya Rais Vladmir Putin: "Inachokifanya Urusi hakikubaliki hata kidogo, na nyumba ya matendo yote ya kibabe ya Urusi ni dhana ya jamii nyingine, ya mtazamo mwingine wa dunia ambavyo ni tofauti kabisaa na falsafa ya Ulaya ya kuheshimiana, ya kuishi pamoja kwa tamaduni mbalimbali na jamii yenye mtazamo mpana."

Umaarufu wa Schulz

Schulz alipata umaarufu kutoka na hotuba alioitoa mwaka 2014, alipolihutubia bunge la Israel la Knesset kwa lugha ya Kijerumani, na kukosoa waziwazi sera ya  serikali ya ujernzi wa mkaazi ya walowezi. Hotuba hiyo ilisababisha vurumai na kupelekea baadhi ya wabunge wa Israel kuondoa bungeni wakipinga hatua hiyo.

Yumkini maneno ya wazi ya Schulz ndiyo yanamfanya kuwa mashuhuri zaidi. Kulingana na uchunguzi wa karibuni wa maoni ya wananchi, umaarufu wake ni sawa na wa Kansela Angela Merkel wa chama cha Christian Democratic Union CDU, na anamzidi kwa mbali kabisaa naibu kansela wa sasa Sigmar Gabriel.

Mwandishi: Jens Thurau
Tafsiri: Iddi Ssessanga
Mhariri: Josephat Charo