1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marufuku kuvuta kwenye vyombo vya usafiri vya umma

P.Martin1 Septemba 2007

Kuanzia tarehe mosi mwezi wa Septemba,nchini Ujerumani ni marufuku kuvuta sigara katika vyombo vya usafiri vya umma na ndani ya majengo ya serikali kuu.Wasiofuata sheria hiyo,watakabiliwa na faini ya hadi Euro 1,000.

https://p.dw.com/p/CB1a
Alama ya kuzuia kuvuta katika treni
Alama ya kuzuia kuvuta katika treniPicha: AP

Vile vile umri wa vijana wanaoruhusiwa kuvuta hadharani na kununua sigara,umeongezwa kuwa miaka 18 badala ya 16.

Hata hivyo,sheria ya Ujerumani inawaruhusu wavutaji katika stesheni kubwa za treni,kutumia sehemu au vyumba maalum vilivyowekwa kwa ajili yao.

Mwaka uliopita,serikali ilishindwa kwa jumla kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani,kwa sababu katiba,iliziruhusu serikali za majimbo 16 ya Ujerumani,kujiamulia suala hilo.

Baadhi ya majimbo,lakini tangu mwezi uliopita,yalijiamulia kupiga marufuku kuvuta sigara katika hospitali na shule.