1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya misaada yaonya janga upembe wa Afrika

Kalyango Siraj2 Julai 2008

Watoto ndio wameathirika mno

https://p.dw.com/p/EUws
Eneo la upembe wa Afrika ambalo linakabiliwa na matatizo mengi mkiwemo vita na ukamePicha: AP

Muungano wa mashirika ya kutoa misaada umetoa mwito wa msaada wa dharura wa chakula na msaada mingine ya kibinadamu kuelekea eneo la upembe wa Afrika,ili kuwasaidia watu millioni 14 wanaokabiliwa na shida ya njaa.

Mashirika tisa ya kutoa misaada,mkiwemo la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto la UNICEF pamoja na mengine ya Umoja wa Mataifa na yasio ya kiserikali,yamesema kuwa mseto wa ukame,migogoro,kupanda kwa bei za vyakula na mafuta,magonjwa pamoja na umaskani vinawalazimisha watu kukabiliwa na janga kubwa.

Mkurugenzi wa ofisi ya UNICEF ya kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika,Per Engebak,ameonya kuwa watoto ndio wanaumia zaidi katika hali hiyo, na kuomba kuchukuliwa mara moja hatua za dharura.

UNICEF linasema kuwa maeneo ambayo yameathirika mno ni Ethiopia na Somalia,ingawa kuna ishara za hali hiyo katika nchi zingine kama vile Eritrea,Djibout,Kenya pamoja na Uganda.

Aidha limesema kuwa kiwango cha utapia mlo nchini Somalia kinazidi asili mia 20,ambacho ni kikubwa zaidi ya kiwango cha asili mia 15 ambayo inachukuliwa kama mbaya inayohitaji msaada wa dharura.

Nalo shirika la mpango wa chakula duniani-WFP limeonya kuwa huenda watu milioni 3 Unusu nchini Somalia wakategemea msaada wa chakula baadae mwaka huu.

Watu malfu kadhaa nchini humo wamekimbia mapigano makali kati ya wapiganaji wa kiislamu dhidi ya serikali ya mpito ya Somalia ilioko mjini Mogadishu.

Mashirika ya kimisaada yanasema kuwa wau zaidi ya milioni 4 wanahitaji chakula cha dharura nchini Ethiopia,mkiwemo watoto laki saba unusu ambao hawana lishe.

Yanmeendelea kuwa Uganda inakabiliwa na hali kama hiyo,nayo Kenya, kwa upande wake,ina watu wanaokadiriwa zaidi ya millioni moja ambao wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Mashirika hayo chini ya kivuli cha chama cha kikanda kinachoratibu shughuli za misaada ya kibinadamu kutoka Nairobi cha Regional Humanitarian Partnersship Team, yameziomba serikali husika pamoja na wahisani kuingilia kati mara moja ili kuokoa maisha ya binadamu na hivyo kuepusha kuongezeka kwa hali mbaya.

Afisa wa shirika la UNICEF,Engebak amesema kuwa, ikiwa hatua hizi muhimu zitachukuliwana serikali pamoja na wahisani wao wa kimataifa kuna mafanikio fulani yatakayofika katika mchakato wa kuepusha janga kwa kipindi kijacho cha miezi kadhaa.