1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya ndege yapakia shehena za misaada na silaha

20 Aprili 2010

Safari kwenye maeneo ya vita au maafa

https://p.dw.com/p/N0xH

Mtandao mpya wa habari ulioanzishwa jana, ndio mtandao wa kwanza duniani wenye shabaha ya kusaka na kugundua shehena zisizo halali na siadilifu zinazopakiwa na ndege zinazokodiwa kusafirisha shehena za uokozi na misaada katika maeneo ya maafa au vita.

Taasisi ya Kimataifa ya Taftishi za Amani mjini Stockholm, Sweden, (SIPRI) kwa ufupi,imearifu kwamba, zaidi ya 90% ya ndege zinazopakia shehena -Cargo- zimegunduliwa kusafirisha silaha pia zikitumiwa kwa shughuli za misaada ya kibinadamu na za kuhifadhi amani tangu na Umoja wa Mataifa ,Umoja wa Ulaya, na hata wanachama wa Shirika la ulinzi la magharibi (NATO).SIPRI yenye makao yake mjini Stockholm, Sweden, imesema ,

"Katika baadhi ya visa hivyo, makampuni ya mashirika ya ndege yanayopakia shehena, yalifirisha tangu shehena za misaada hata silaha katika eneo lile lile la ugomvi."

Makampuni hayo ya ndege yanayopakia shehena yaliotajwa, ni pamoja na Bluebird Aviation,Aerostan,Air Koryo,Ababeel Aviation,Badr Airlines,Juba Air cargo,Aerocom,Trans-Attico na United Arab Airways.Baadhi ya mashirika hayo ya ndege yalikodiwa kusaidia mipango ya kijeshi ya vikosi tangu vya Marekani hata vya NATO tangu nchini Afghanistan hata Iraq.

Akiulizwa iwapo mashirika ya Umoja wa Mataifa ,Umoja wa Ulaya na nchi zanachama wa NATO, zilitumia mashirika hayo ya ndege yanayopakia shena yakijua yanachopakia au kwa ndio pekee yenye uwezo wa kutoa huduma hizo kwa bei nafuu,Hugh Griffiths wa shirika la SIPRI aliliambia shirika la habari la IPS kwamba, itakua shida kuthibitisha kuwa mashirika hayo ya ndege yaliotajwa katika ripoti za UM na nyenginezo yanatumiwa kwa kujua.

Baadhi ya nyakati mfano katika visa vya safari za kuhifadhi amani za vikosi vya UM au Umoja wa Afrika nchini Sudan, hakujakuwapo njia nyengine. Lakini, aliongeza Griffiths, kwa jumla, matatizo haya yanazuka kutokana na kutoelewa .

Nchini Sudan, ambako Kamati ya vikwazo ya UM juu ya Dafur, ilipendekeza kiasi ya mashirika 6 ya carago kupigwa marufuku, vikosi vya kuhifadhi amani vya UA na UM viliendelea kutumia huduma zao.Na hii ,licha marufuku ya UM iliochapishwa katika waraka wa Baraza la Usalama ambao upo katika mtandao.

"Kwahivyo, si kuwa Kamati ya vikwazo ya UM haichukui juhudi za kutosha, lakini tatizo liko upande mwengine.Ukosefu wa taarifa na kutojua"-asema mjumbe huyo wa SIPRI, Griffiths.

Mwandishi: Ramadhan Ali/IPS

Uhariri:Abdul-Rahman