1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mateka mmoja wa Kijerumani yuhai

P.Martin22 Julai 2007

Kufuatia kifo cha mateka mmoja wa Kijerumani nchini Afghanistan,serikali ya Ujerumani sasa inashughulika na juhudi za kupata uhuru wa mateka wa pili.

https://p.dw.com/p/CB2c
Wahandisi wa Kijerumani walitekwa nyara Wilaya ya Wardak nchini Afghanistan
Wahandisi wa Kijerumani walitekwa nyara Wilaya ya Wardak nchini AfghanistanPicha: AP GRaphics/DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier,alipozungumza na waandishi wa habari mjini Berlin alisema:

“Sasa kilichokuwepo ni kujitahidi kuchukua kila hatua inayowezekana kibinadamu na inayowajibika, ili kuokoa maisha ya mateka wa pili.“

Hapo awali,msemaji wa Taliban alidai kuwa kundi hilo la wanamgambo limewauawa mateka wote wawili. Wahandisi wawili wa Kijerumani na wafanyakazi wenzao watano wa Afghanistan,walitekwa nyara katikati ya Afghanistan,walipokuwa wakifanya kazi katika mradi mmoja wa bwawa.