1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi yaanza kutolewa Comoro

27 Desemba 2010

Wagombea wawili kati ya watatu wa uraisi na magavana wanaowaunga mkono maraisi hao wanaonesha kufanya vizuri kwenye uchaguzi huo. Kambi ya upinzani imesema uchaguzi haukuwa wa haki hasa katika kisiwa cha Ndzuwani

https://p.dw.com/p/zqEJ

Matokeo ya awali kufuatia uchaguzi wa rais uliofanyika jana katika visiwa vya Comoro yanatarajiwa kuanza kutolewa leo. Wapiga kura nchini humo, walipiga kura kumchagua mrithi atakayechukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake Ahmed Abdallah Sambi, katika uchaguzi ambao wagombea wa upinzani wanadai kuwa ulitawaliwa na vitendo vya udanyanyifu.

Kiongozi wa upinzani katika kisiwa cha Njuwani, Mohamed Djanfaari amelituhumu jeshi la nchi hiyo kwa kuongeza kura zisizo halali katika masanduku ya kura. Aidha ameitaka Jumuiya ya kimataifa na mahakama ya katiba kuufuta uchaguzi huo.