1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauaji zaidi Syria

Oumilkher Hamidou8 Mei 2011

Licha ya serikali kuweka marufuku ya kuandamana bila ya kibali, hali ya mambo inazidi kuharibika nchini Syria, huku vikosi bvya serikali vikiendelea kuwashambulia waandamanaji kwenye miji kadhaa nchini humo.

https://p.dw.com/p/11Bd7
Waandamanaji mjini Banias
Waandamanaji mjini BaniasPicha: dapd

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Syria wanasema watu sita wameuwawa wakati vikosi vya serikali vilipouvamia mji wa bandari wa Banias.

Miongoni mwa waliouwawa ni waandamanaji wanne wa kike ambao walikuwa wakidai kuachiliwa huru kwa watu waliokamatwa.

Madarzeni ya vifaru na magari ya deraya yanaripotiwa kuingia katika mji huo wa kaskazini magharibi ambapo wakaazi wake walishikana pamoja kuunda kinga kujaribu kuzuwiya operesheni hiyo ya kijeshi.

Makundi ya haki za binadamu yanasema hadi sasa, watu 600 wameuwawa wakati wa maandamano ya nchi nzima kudai kukomeshwa kwa utawala wa kidikteta wa Rais Bashar al- Assad.