1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu kulihutubia bunge la Marekani

2 Machi 2015

Mauwaji ya mwanasiasa wa upinzani,Boris Nemzow nchini Urusi,hotuba ya waziri mkuu wa Israel katika bunge la Marekani,na kitisho cha mashambulio ya kigaidi mjini Bremen ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/1EjiX
Umati wa warusi waomboleza kuuliwa kiongozi wa upinzani Boris NemzowPicha: DW/Y. Wischnewetzkaya

Tuanzie lakini Urusi ambako orodha ya wapinzani wanaouliwa inazidi kuwa ndefu.Gazeti la "Thüringische Landeszeitung" linaandika:"Boris Nemzow alimtuhumu Vladimir Putin kufuata siasa ya mauwaji nchini Ukraine.Yeyote yule aliyemuuwa Nemzow kwa hivyo,anaamini alikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo kwa niaba ya Putin.Hata hakuhitaji kupewa amri.Hata kama Putin kitendo kama hicho hajakifurahikia,asingeweza lakini kutokana na hali namna inavyochemka nchini, kukizuwia.Mauwaji ya Nemzow yamewateremsha wengi majiani.Baada ya risasi kufyetuliwa hawakutaka kujifungia kwa woga majumbani mwao,badala yake wameyatumia maandamano yaliyoitishwa,kubainisha huzuni na msiba wao.Maandamano ya jana jumapili yanapaswa kugeuka msimu wa kiangazi kwa upande wa upinzani.Sasa lakini muda mfupi baadae risasi hizo zilizosababisha kifo zinatoa ushahidi wa hali inayotisha iliyoko nchini Urusi.Na mara kumbukumbu zinarejea za wale waliopoteza maisha yao kwasababu ya kupigania maisha bora.

Msimamo wa Netanyahu kuhusu mradi wa kinuklea wa Iran wautikisha uhusiano pamoja na Marekani

Gazeti la "Trierischer Volksfreund linamulika madowa katika uhusiano kati ya Israel na Marekani.Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaelekea Marekani ambako kesho anatarajiwa kulihutubia bunge la nchi hiyo Congress.Ziara hiyo inafanyika bila ya ridhaa ya ikulu ya Marekani.Gazeti linaendelea kuandika:"Hajawahi pengine Benjamin Netanyahu kutoa hotuba muhimu zaidi ya hiyo.Kesho waziri mkuu huyo wa Israel amepania kuonya dhidi ya hatari ya mradi wa kinuklea wa Iran.Kichini chini hatoitupa fursa ya kumshutumu rais Barack Obama,anajidanganya akiamini kwamba Teheran itaachilia mbali mipango yake ya siri ya kutengeneza silaha za kinuklea.Makubaliano rais Barack Obama anayopanga kuyafikia pamoja na Iran,Netanyahu anayaangalia kuwa ni makosa makubwa.Hapo lakini anarudia tu yale ambayo tayari ameshayasema.Na licha ya hayo hotuba yake ya kinga mbele ya bunge la Marekani-Congress inatishia kuutia dowa uhusiano wa Israel na Marekani-tukio ambalo halijawaahi kushuhudiwa tangu miongo kadhaa iliyopita.

Israel Benjamin Netanjahu auf dem Weg nach Washington
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkewe Sarah wakiwa njiani kuelekea WashingtonPicha: Getty Images/Amos Ben Gershom

Kitisho cha mashambulio ya wafuasi wa itikadi kali caenea pia Ujerumani

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu kitisho cha kutokea mashambulio ya kigaidi katika mji wa kaskazini Bremen.Gazeti la "Stuttgarter Nachrichtren" linaanadika:"Baada ya mashambulio mijini Copenhagen,Brussels na Paris,maafisa wa idara za usalama nchini Ujerumani nao pia wako katika hali ya tahadhari mtindo mmoja.Kama kuingilia kwao katika sherehe za karinivali mjini Braunschweig au hivi karibuni mjini Bremen kumeepusha kweli balaa la umwagaji damu-hakuna anaeajuwa kwa uhakika.Kwa vyovyote vile ilivyo,yaonyesha kana kwamba hatari ya shambulio la kigaidi la wafuasi wa itikadi kali haitokani na kundi la kigaidi linaloeneza propanga zake kupitia mtandao au vyombo vyenginevyo vya mawasiliano.

Bremen Terrorwarnung
Jengo la utamaduni wa kiislam mjini Bremen lilivamiwa na kusachiwa na polisi kufuatia rirpoti za kitisho cha mashambulio ya kigaidi ya wafuasi wa itikadi kaliPicha: picture-alliance/dpa/C. Jaspersen

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman