1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Afya wakutana kujadili Ebola

Mjahida2 Julai 2014

Mawaziri wa afya wa nchi 11 za afrika Magharibi na wataalam wa kimataifa wanatathmini kuanzisha mpango maalum wa kukabiliana na ugonjwa hatari wa homa ya Ebola.

https://p.dw.com/p/1CURP
Baadhi ya madaktari wasio na mipaka wakiubeba mwili wa mtu aliyefariki kutokana na homa ya Ebola
Baadhi ya madaktari wasio na mipaka wakiubeba mwili wa mtu aliyefariki kutokana na homa ya EbolaPicha: Seyllou/AFP/Getty Images

Kulingana na takwimu za shirika la afya duniani watu 759 wameathirika kutokana na ugonjwa huo na wengine 467 wamekufa katika nchi 3 ambazo ni Sierre Leone, Guinee na Liberia. Takwimu hizo ni sawa na ongezeko la watu 129 katika kipindi cha wiki moja, ikiwa ni ishara ya ugonjwa huo kuzidi kuzagaa baada ya kuonekana kutulia katika mwezi april.

"Ni ugonjwa unaoambukiza na kuuwa haraka " ilisema taarifa ya shirika la afya duniani WHO muandalizi wa mkutano huo unaofanyika katika mji mkuu wa ghana Accra.

"Maamuzi ya mkutano huo, yatakuwa muhimu kukabiliana kwa sasa na ugonjwa huo na baadaye kwa magonjwa mengine ya kuambukiza" ilisema taarifa hiyo.

Kufuatia ongezeko la idadi ya vifo na ya watu wanao ambukizwa virusi vya Ebola, shirika la afya duniani " lilitahadharisha "

Mgonjwa wa Ebola ashughulikiwa na wataalamu
Mgonjwa wa Ebola ashughulikiwa na wataalamuPicha: picture alliance/AP Photo

na kusema kuwa " hatua muhimu zahitajika " ili kukabiliana na ugonjwa huo unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwengine na kuua.

Juni 23, shirika ya kimataifa la madaktari wasio na mipaka lilitahadharisha kuwa maradhi hayo sasa " hayadhibitiwi " na yanatishia kuyakumba maeneo mengine.

Mwito ambao ulipelekea, shirika la afya kuwatuma wataalam 150 Guinee ambako ugonjwa huo ulionekana kwa mara ya kwanza mwezi januari na kusambaa sehemu nyingine. Licha ya juhudi za WHO na mashirika mengine ya kimataifa, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanao ambukizwa na vifo katika wiki kadha za nyuma, taarifa hiyo iliongeza kusema.

" WHO, linahofu juu ya maambukizi ya ugonjwa huo katika nchi za jirani na hata kwenye ngazi ya kimataifa katika siku za mbele ", alisema Daktari Luis Sambo, mkurugenzi wa kikanda wa umoja wa mataifa katika bara Afrika.

Hatua kali zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti Ugonjwa wa Ebola

"Awamu hii ya pili ya ugonjwa huo iliyosababisha idadi ya vifo kuongezeka katika wiki za nyuma imesababishwa na kupuuzwa uhamasishaji katika nchi hizo 3 za Afrika magharibi zinazo kumbwa na virusi hivyo, wakati ugonjwa ulikuwa umeonekana kupunguwa katika mwezi April ", aliiambia AFP Pierre Formenty mtaalam kwenye WHO.

"Tukio moja tu laweza kusababisha maambukizi" alisema na kwamba " Hatua kali zaweza kuudhibiti ugonjwa huo".

Wanaudhuria mkutano huo wa mawaziri wa afya na maafisa wa ngazi ya juu kutoka nchi za Guinee, Liberia, Sierre Leone, Cote d´Ivoire, DRC, Gambia, Ghana, Guinee Bissau, Mali, Senegal na Uganda.

Moja ya wataalamu katika chumba cha wanakowekwa wagonjwa wa Ebola
Moja ya wataalamu katika chumba cha wanakowekwa wagonjwa wa EbolaPicha: Cellou Binani/AFP/Getty Images

Pamoja na washirika wa WHO katika kukabilia na ongezeko la Ebola, ikiwa ni pamoja na mashirika ya madini, Madaktari wasiyo na mipaka, wale wa kituo cha uchunguzi wa maradhi mbali mbali katika nchi za joto, wale kutoka Umoja wa ulaya na marekani.

Virusi vya Ebola vinavyo sababisha homa ya uvujaji wa damu, kutapika na kuharisha jina lake latokana na mto mmoja kaskazini mwa DRC, viliko kudunguliwa kwa mara ya kwanza 1976, vikiwa havina hadi sasa chanjo.

Kiwango chake cha kuuwawa cha kadiriwa asilimia 25 hadi 90 kwa mwanaadam kutokana na aina ya virusi.

Mwandishi / Amida ISSA / Reuters/AFP

Mhariri /Yusuf Saumu