1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa maendeleo wa umoja wa ulaya wakutana Bruxelles

Hamidou, Oumilkher13 Mei 2008

Watawala wa kijeshi wa Myanmar watakiwa wawaruhusu watumishi wa mashirika ya kimataifa wawahudumie wahanga wa kimbunga Nargis

https://p.dw.com/p/Dz80
Misaada kwa wahanga wa kimbunga NargisPicha: AP


Mawaziri wa maendeleo wa Umoja wa ulaya wamekutana hii leo mjini Bruxelles kujaribu kuwatanabahisha viongozi wa Myanmar waruhusu misaada ya kimataifa iingie nchini humo ili kuwahui wahanga wa kimbunga Nargis.


"Tunachokitaka hasa ni kuushinikiza utawala wa kijeshi ukubali kuwahifadhi wananchi wake"ezea waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Heidemarie Wieczoreck -Zeul,alipowasili katika mkutano huo wa dharura mjini Bruxelles.


Lakini  yadhihirika kana kwamba bado hadi dakika hii mawaziri wa maendeleo wa nchi za umoja wa ulaya bado hawajagundua njia inayofaa kufuatwa-majadiliano yanaendelea kati ya "msimamo mkali" unaotetewa na Ufaransa iliyoshauri Umoja wa mataifa upitishe azimio ili kuilazimisha serikali ya mjini Rangun ikubali misaada ya kimataifa na msimamo  wa tahadhari  unaotetewa na baadhi ya nchi za umoja huo.


Pendekezo la Ufaransa,linatokana na muongozo wa Umoja wa mataifa kuhusu kuhusu "wajib wa ulinzi"-kifungu cha maneno kinachohalalisha kuibngilia kati ili kuhui maisha ya binaadam. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner ni mmojawapo wa waasisi wa kifungu hicho cha maneno.


Muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana anaonyesha kuunga mkono msimamo huo wa Ufaransa.

Bwana Solana anasema:


"Bila ya shaka tutabidi tutumie njia zote zilizoko kuwasaidia wahanga hao.Muongozo wa Umoja wa mataifa unaruhusu ikiwa hakuna njia nyengine ,ili kuweza kuingiza misaada ya kiutu  katika nchi inayokumbwa na balaa kama hili lililotokea Myanmar na ambako viongozi hawataki kuruhusu misaada iingizwe haraka."


Siku 11 baada ya janga baya kabisa la kimaumbile kupiga nchini ghumo,janga lililogharimu maisha ya watu 62 elfu na wengineo wasiojulikana waliko,watawala wa kijeshi wa Myanmar wanaendelea kupinga watumishi wa mashirika ya kimataifa ya misaada ya kiutu wasiingie kwa wingi kuwahudumia watu milioni moja na nusu walioangukia mhanga wa kimbunga Nargis.


Ikiwa viongozi wa kijeshi wataendelea na msimamo huo,kisa hicho kinaweza kulinganishwa na uhalifu dhidi ya ubinaadam" amesisitiza katibu wa dola wa Hispania anaeshughilikia siasa ya anje Diego Lopez Garrido.


Hhata hivyo ametoa mwito wa busara akisema "hawataki kukorofisha mambo.


Mawaziri hao 27 wa maendeleo wanatazamiwa kuwasihi kwa hivyo viongozi wa kijeshi wa Myanmar wakubali watumishi wa mashirika ya kimataifa waingie nchini humo.

Umoja wa Ulaya unategemea uungaji mkono wa mataifa jirani ya eneo hilo.

Mkutano huu wa dharura umeitishwa na kamishna wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya Louis Michel anaepanga kwenda Bankok akiwa na matumaini ya kuweza baadae kuitembelea Myanmar.


Louis Michel anasema ziara yake ni ya kiutu na sio ya kisiasa.


Umoja wa ulaya umeiwekea Myanmar,tangu mwaka 1998 vikwazo vya silaha,marufuku ya kupaztiwa viza baadhi ya viongozi wa nchi hioyo na kuzuwiliwa mali zao zilizowekwa katika nchi za ulaya,pamoja pia na kupigfwa marufuku biashara ya mbao,maadini ya dhahabu na almasi na maadini mengineyo. 



►◄