1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Ujerumani na China kukutana leo

Halima Nyanza(ZPR)28 Juni 2011

Mawaziri wa Ujerumani na China wanakutana hii leo mjini Berlin, kwa mazungumzo ya pamoja ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika, ambapo ajenda kuu inatarajiwa kuwa ushirikiano wa kibiashara baina ya pande mbili

https://p.dw.com/p/11kVE
Kansela Angela Merkel na Waziri mkuu wa China Wen JiabaoPicha: dapd

Mawaziri hao wa China wamo katika ujumbe wa Waziri mkuu wa nchi hiyo, Wen Jiabao, ambaye yuko Ujerumani kwa ziara ya siku mbili.

Aliwasili jana jioni na kupokewa na Kansela Angela Merkel.

Berlin Chinas Ministerpräsident Wen Jiabao und Bundeskanzlerin Angela Merkel
Waziri mkuu wa China Wen Jiabao na Kansela MerkelPicha: dapd

Awali,  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle alisema kwamba atagusia suala la haki za binadamu nchini humo wakati wa ziara hiyo ya Waziri mkuu wa China, hapa nchini.