1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Ulaya wajadili uhamiaji

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYPC

BRUSSELS

Mawaziri wa sheria na mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Brussels Ubelgiji kujadili suala la uhamiaji.

Takriban watu milioni mbili hukimbilia Umoja wa Ulaya wa nchi wanachama 27 kwa kupitia nchi nyengine kila mwaka. Serikali nyingi huwatumia wahamiaji kuziba pengo la uhaba wa wafanyakazi na kufidia idadi ya wananachi wao inayozeek.Katika kikao cha faragha mjini Brussels mawaziri hao wanategemewa kuelezea misimamo ya nchi zao na kutathmini mapendekezo kadhaa yanayowasilishwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya.

Mapendekezo hayo ni pamoja na mipango ya kuwepo kwa Kadi ya Buluu itakayotumika katika nchi zote za umoja huo ikiwa ni kibali cha kuruhusu kufanya kazi na mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa kutoka nchi zilio nje ya Umoja wa Ulaya na kuweka vikwazo vikali kwa kampuni zenye kuwajiri wahamiajji walio kinyume na sheria.